Maumivu yamepona,Notre-Dame ya Paris imerudi kwa watu wa Mungu!
Na Delphine Allaire – Mwakilishi maalum huko Paris
Ni kwa njia ya ibada adimu na ya kale ya upako wa Mafuta ya Krisma ambapo Askofu Mkuu wa Paris, Laurent Ulrich, alipoweka wakfu madhabahu kuu ya Kanisa Kuu la Notre-Dame wakati wa Ibada ya Misa Takatifu, tarehe 8 Desemba 2024, katika maadhimisho ya Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa. Dominika ya II Majilio. Kwa kupaka mafuta matakatifu juu ya madhabahu ya shaba iliyosafishwa, kabla ya kufukiza umati wa waamini Askofu Mkuu huyo aliweka wakfu mahali pa katikati pa Kanisa kuu, madhabahu iliyoharibiwa na moto kunako 2019.
Sasa ina hazina mpya, ya masalio ya watakatifu watano waliounganishwa kwa njia moja au nyingine na Kanisa la Paris, kama vile: Mtakatifu Charles de Foucauld, Catherine Labouré au shahidi wa Kiromania Vladimir Ghika wa asili ya Kiorthodox. Hawa watasimamia Kanisa kuu ambalo limechomoza kutoka katika miali ya moto, kama wale walioalikwa katika litania iliyosomwa na mapadre 170 walioudhuria katika hafla hiyo.
Furaha inaongezeka tena
Askofu mkuu wa Paris alisema katika ibada iliyoadhimishwa ndani ya Kanisa kuu lililorejeshwa na kusafishwa kwamba “ Asubuhi ya leo, maumivu ya tarehe 15 Aprili 2019 yamefutwa. Hii ilikuwa ni Liturujia ambayo hatimaye alichukua umiliki wa Kanisa lake kuu, akiwa ameteuliwa kwenda Paris miaka mitatu tu baada ya moto kuteketeza. Miaka mitano baada ya uharibifu huo, kingo za Seine zilipata waamini na mioyo myepesi na iliyohakikishiwa zaidi, licha ya mvua na upepo, wenye nguvu sana kiasi cha kutaka kuzima moto milele. Jeraha limepona. Ndani ya Kanisa kuu, maajabu hayo yanafikia kiwango chake cha juu kabisa kutokana na kiwiko cha Wagothci na kumeta meta kwa madirisha ya vioo, ambavyo milipuko yake ya rangi ilikuwa ikichomoza kuelekea kwenye kasula za makuhani.
Hili pia linadhihirishwa na sura ya wageni 2,500 waliohudhuria sherehe kati ya tarehe 7 Desemba usiku na 8 Desemba. Waamini au wasioamini, kuna mitazamo mingi iliyoinuliwa mbinguni huko Notre-Dame, wengine hata wamefunikwa na machozi. Hisia kali na matumaini pia zilizowasilishwa na Askofu Mkuu Ulrich: “Kila bonde litajazwa, kila mlima na kila kilima kitashushwa; vijia vyenye vilima vitanyooka, vinjia vya miamba vitasawazishwa; na kila kiumbe hai kitauona wokovu wa Mungu,” alisema katika mahubiri yake. Waliokuwepo ni Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, mkewe Brigitte, na baadhi ya wakuu wa nchi waliosalia katika Ville Lumière baada ya sherehe siku moja kabla ya Misa kuu.
Mahubiri ya Askofu Mkuu
"Acha vazi lako la huzuni na taabu, Notre-Dame, na uvae vazi la utukufu wa Mungu milele, jivike vazi la haki ya Mungu", aliongeza Askofu Mkuu huyo, akialika kila mtu kujiruhusu kuongozwa "kwa furaha kuu, zawadi nzuri zaidi ambayo Mungu hutoa ya uwepo wake wa upendo, ya ukaribu wake na maskini zaidi, ya nguvu zake za kubadilisha katika sakramenti". “Acheni mustaajabishwe na Mungu,” aliendelea Ulrich, alipigiwa makofi kwa muda mrefu alipotoka katika Kanisa kuu na katika uwanja wa kanisa na makasisi wa jiji hilo. Pia waliokuwepo kwenye Misa hiyo walikuwa askofu mkuu mstaafu, Michel Aupetit, ambaye alikumbana moja kwa moja na janga hilo, mtangulizi wake André Vingt-Trois, na Balozi wa Vatican nchini Ufaransa,Askofu Mkuu Celestino Migliore.
Viongozi kadhaa wa Makanisa ya Mashariki na Kiorthodox pia walitaka kushiriki kusimama karibu na Mama katika siku hii iliyowekwa kwake. Miongoni mwao, Patriaki wa Maronite Bechara Räi, mjumbe wa Patriaki Bartholomew, Metropolitan Emmanuel wa Chalcedon, na Tawadros II, Patriaki wa Kiorthodox wa Kikoptic. Uwepo wa kiekumene ambapo Askofu Mkuu anayeimamia umoja wa Kikristo alisema alifurahishwa sana nao, na pia kuweza kuingia Notre-Dame tena: "Inahisi kama ninarudi nyumbani, lakini imesafishwa. Ni Mama Kanisa yuleyule, lakini limegeuzwa sura na mchezo wake wa nuru, kuonekana tena kwa chombo na watu wa Mungu ambao watakijaza kuanzia sasa.
Watoto katika Notre-Dame kubwa
Hatimaye, hawakuweza kukosa Misa ya uzinduzi: waamini, wagonjwa, maskini, watu wa kujitolea waliokusanyika pamoja na vyama sita vilivyoalikwa na askofu mkuu. Miongoni mwa hawa Prisca, mfanyakazi wa kujitolea wa Ofisi ya Kikristo ya watu wenye ulemavu, ambaye alifafanua tukio la leo kama "tukio la karne": "Kwa makusudi sikuangalia picha yoyote kabla ya wikendi hii", alitabasamu na vyombo vya habari vya Vatican, akisema, kuwa ameguswa na amejazwa shukrani. “Mungu hualika walio wadogo zaidi na hukaribisha walio dhaifu zaidi. Jamii zetu zinakaribisha watu walio katika mazingira magumu.
Sisi tulio na ulemavu tuna kitu cha kusema kwa ulimwengu, kwa hivyo uwepo wetu unakaribishwa sana", anasisitiza Florence, ambaye pia anafanya kazi katika ofisi hiyo hiyo. Ishara ya ukaribu na watu walio katika mazingira magumu, mbali na mazulia ya kidiplomasia na uboreshaji wa kidunia, ilikuwa ni mpango wa Jimbo kuu la Paris la Chakula cha maskini 150 wa jiji hilo. Wakati huo ulifanyika baada ya Misa chini mahema ya Chuo cha Bernardin.