Papa:Mti na ishara za tukio la kuzaliwa kwa Kanisa ambalo kuna nafasi kwa wote!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 7 Desemba 2024 aliwakaribisha kwa ukarimu viongozi wa kiraia na wa kikanisa waliofika katika Ukumbi wa Paulo VI katika siku ya kuwakilisha zawadi zao za kutengeneza Pango na mapambo ya mti wa Noeli katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, pamoja na mapambo na Pango la Ukumbi wa Paulo VI, pia hata Wawakilishi Maalum wa Rais wa Palestina, Mheshimiwa Mahmoud Abbas - ambaye alikuja hapo mara kadhaa, Mkuu Mkoa wa Friuli Venezia Giulia na Mkuu Mkoa Trento, Askofu Mkuu wa Gorizia, Mameya wa Grado na Ledro. Papa alisema kuwa "Sherehe kuu ya mti Noeli ni ya kushangaza. Mti uliokatwa kwa kufuata kanuni za kiikolojia za uingizwaji wa asili ya msitu, hunazaa ishara za miaka mingi, tabaka nyingi za shina kubwa, zile za kizamani ambazo zimewapa maisha vijana, na kuwa kuwafunika na kulinda yale ya kale, yainukayo pamoja ili kwenda juu.
Papa alisema kuwa hiyo inaweza kuwa taswira nzuri ya Kanisa, watu na mwili, ambamo nuru ya Kristo inaenea ulimwenguni kote kutokana na mfululizo wa vizazi vya waamini wanaokusanyika kuzunguka asili moja, ambayo ni Yesu. Kwa wale wa kale walitoa uhai kwa ajili ya vijana, wanawakumbatia na kuwalinda wale wa kale, wakiwa kwenye utume duniani na kuelekea Mbinguni. Hivi ndivyo watakatifu wa Mungu, watu waaminifu wanavyosonga mbele. Katika kivuli cha mti mkubwa wa, eneo la pango, kutoka Grado, moja ya nyumba za wavuvi ambazo zilijengwa kwa udongo na mwanzi na ambapo wenyeji wa visiwa vidogo vya rasi, walishiriki, wakati wa kazi ngumu ya uvuvi, furaha na huzuni ya maisha ya kila siku. Alama hii pia inazungumza nasi juu ya Noeli ambayo Mungu anakuwa mwanadamu ili kuwa na sehemu kamili katika umaskini wetu, akija kujenga Ufalme wake duniani si kwa njia zenye nguvu, la! bali kupitia rasilimali dhaifu za ubinadamu wetu, zilizosafishwa na kuimarishwa kwa nguvu ya neema yake.
Kuhusu tukio la Kuzaliwa kwa Yesu, kuna ishara nyingine ambayo Papa Francisko alipenda kuonesha ile ya kijumba kilichozungukwa na maji na kwenda huko unahitaji "mtumbwi wa kawaida ambao unakuwezesha kuelea juu ya maji ya kina. Na hata kumfikia Yesu unahitaji mtumbwi ambao ni Kanisa. Haufikii huko peke yakokamwe -huifikii bali, unapafikia katika jamii, kwenye mtumbwi huo mdogo ambao Pietro anaendelea kuendesha na kwenye bodi akwa kujibamiz ndani kidogo, kwa sababu kuna nafasi kila wakati kwa wote.” Papa amekazia kusema kuwa “Kanisani daima kuna nafasi kwa kila mtu. Wengine wanaweza kusema, “Lakini vipi kuhusu wenye dhambi?”Hawa ndio wa kwanza, ndio waliobahatika, kwa sababu Yesu alikuja kwa ajili ya wenye dhambi, kwa ajili yetu sisi sote, si kwa ajili ya watakatifu. Kwa kila mtu. Msisahau hili. Wote, wote !na kila mtu ndani," Papa alisisitiza.
Hatimaye, Papa ametaka kutazama Pango la Kuzaliwa kwa Yesu ya Bethlehemu, lililojengwa katika nchi ambayo Mwana wa Mungu alizaliwa. Lile ni tofauti na kila mmoja wao, lakini yote hubeba ujumbe sawa wa amani na upendo ambao Yesu aliotuachia. Mbele yake, tunakumbuka akina kaka na dada ambao, badala yake, papo hapo na katika sehemu nyinginezo za ulimwengu, wanateseka kutokana na janga la vita. Kwa machozi machoni mwetu tunainua maombi yetu ya amani. Papa amekazia kusema kuwa: "Kaka na dada, hakuna kufanya vita tena, hakuna vurugu tena”! Ninyi mnajua kuwa moja ya vitega uchumi vinavyotoa mapato mengi hapa ni kwenye kiwanda cha kutengeneza silaha? Kupata kuua ... lakini kwa nini? Hakuna vita tena!” Na kuwe na amani duniani kote na kwa watu wote ambao Mungu anawapenda (Lk 2:14)! Papa amewashukuru tena kufika kwao na kwa zawadi zenu za thamani. Ameishukuru Kurugenzi ya Miundombinu na Huduma ya Vatican kwa kujitolea kwa ukarimu na bidii ambayo iliandaa haya yote. Aliwabariki, familia zao na wananchi wao wote. Na kuwaomba tafadhali, wasisahau kumuombea, lakini wasiombe dhidi yake.