Tafuta

Kimbunga  Chido nchini Msumbiji. Kimbunga Chido nchini Msumbiji. 

Papa Francisko:akumbuka maafa ya kimbunga Chido,Msumbiji na Mayotte,Ufaransa

Mwishoni mwa katekesi katika Ukumbi wa Paul VI,Papa alikumbuka maafa ya kimbunga kikali Chido nchini Msumbiji na kile cha Mayotte huko Ufaransa.Alizindua wito mpya kwa ajili ya amani duniani na kurudia kusema kwamba vita daima ni kushindwa.Asante kwa makaribisho mazuri huko Corsica na kuwataka mahujaji wa Poland kukumbuka wakimbizi wa Ukraine wakati huu wa Noeli.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa washiriki elfu saba waliokusanyika katika Ukumbi wa Paulo VI ili kushiriki katika katekesi yake, mwishoni kabla ya Noeli Papa Francisko tarehe 18 Desemba 2024  kati ya miito yake  ya  baada ya katekesi alikumbuka wenyeji wa visiwa vya  Mashariki mwa Msumbuji kwa kimbunga kikali ‘Chido’ na huko Mayotte nchini Ufaransa vilivyoharibiwa katika siku za hivi karibuni na, ambacho wanaogopa labda kuna maelfu ya waathirika. “Mungu awape pumziko lao waliopoteza maisha, msaada unaohitajika kwa wenye shida na faraja kwa familia zilizoathirika.”

Vita ni kushindwa

Papa Francisko hachoki kukaribisha zawadi ya amani na hufanya hivyo kwa kutaja "Ukraine iliyoteswa" wakati akizungumza na  waamini wa Poland na zaidi ya yote wakati wa kusalimiana na vikundi vya Italia: “Tusiwasahau watu wanaoteseka na vita: Palestina, Israel, na wote wanaoteseka, Ukraine, Myanmar... Tusisahau kuombea amani, vita viishe. Tusisahau, vita daima ni kushindwa, daima! Vita daima ni kushindwa.” Mila na tamaduni za Noeli ni ishara ya nia ya kukaribisha na roho ya ukarimu. Papa alikumbuka hili wakati anatumaini kwamba kutakuwa na tukio la kuzaliwa majumbani. Ni kipengele muhimu cha hali yetu ya kiroho na utamaduni wetu, njia ya kusisimua ya kumkumbuka Yesu ambaye alikuja 'kuishi kati yetu.' Na kati ya tamaduni za wakati huu, alikumbuka pia, katika salamu zake kwa wanahija wa Kipoland, kwamba oplatek, yaa mkate wa Noel  unamwegwa nchini. "Ishara hii ya upendo, amani na msamaha  ni kielelezo cha moyo ulio wazi kwa wale unaokutana nao kwenye njia yao.  Wito wa Papa Fransisko ni kudumu katika kumbukumbu, zaidi ya yote, ya maskini, wapweke, na wahanga wa mafuriko.

Papa atoa shukrani za makaribisho huko Corsica

Katika salamu zake kwa mahujaji wanaozungumza lugha ya Kifaransa, Papa aliwageukia wanafunzi wa shule mbalimbali za Paris na Dijon, pamoja na waamini wanaosindikiza masalia ya Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu. Kisha alikumbuka safari ya kwenda Corsica Dominika tarehe 15 Desemba 2024 na kusisitiza makaribisho ya uchangamfu sana alioupokea. Papa aAlisema alivyoshangazwa sana na mahamasisho ya watu na kwa maoni kwamba hapo imani si jambo la kibinafsi." Kisha mawazo yake kuhusu idadi kubwa ya watoto waliokuwepo Ajaccio, jambo ambalo tayari alikuwa ameakisi kwa waandishi wa habari wakati wa kurudi Roma kwamba  "ni furaha kubwa na tumaini kubwa!".

Wakati wa Noeli wasiwasahau wazee peke yao

Katekesi inayohusu ukoo wa  Yesu inawahusu wahenga, kwa njia hiyo ni kwa babu na bibi  zetu na kwa utajiri wa wazee wote ambapo, Papa Francisko aliendelea katika salamu zake kwa waamini wanaozungumza Kireno. “Ni fursa ya kusisitiza thamani ya wale ambao ni wazee, na kufanya hivyo siku baada ya siku yao ya kuzaliwa kwamba “Ni zawadi kutoka kwa Mungu ya kushukuriwa na kutunzwa. Tusiwaruhusu wajikute peke yao wakati wa sikukuu zijazo za Noeli,” Papa alisisitiza.

Baada ya katekesi
18 December 2024, 15:28