Tafuta

2024.12.11 Papa na Jukwaa la Kiuchumi la Binadamu. 2024.12.11 Papa na Jukwaa la Kiuchumi la Binadamu.  (Vatican Media)

Papa Francisko:lazima kuhamasisha mahitaji ya uchumi endelevu ya binadamu!

Baba Mtakatifu amekutana tarehe 11 Desemba 2024 na washiriki wa Jukwaa l la Uchumi wa Binadamu linaloendelea siku hizi jijini Roma.Katika hotuba yake amesisitiza juu ya kuelekeza mtazamo kwa watu katika nyanza zao zote ili kupambana na umaskini,kurejesha utu wa waliotengwa,kuwatunza katika nyumba ya kawaida ya wote.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 11 Desemba 2024 akikutana na Washiriki wa Jukwaa la I la Uchumi wa Binadamu amewasalimia akiwa na furaha ya kuwakaribisha katika hafla ya Kongamano  hilo, ambalo linafanyika Roma siku hizi.  Mkutano wao, unaohusu masuala muhimu ya kiuchumi na kijamii, ambayo yamejikita katika mada ya uendelevu wa binadamu. Papa amesema kuwa “Utafutaji wa maendeleo endelevu na fungamani ya  binadamu ni muhimu kwa kuhakikisha na kukuza manufaa ya wote kwa wote. Kwa sababu hiyo, ni muhimu kumweka mwanadamu katika moyo wa mahangaiko na shughuli zetu zote, alisema Papa Francisko.

Dira ya Kimataifa

Askofu wa Roma aidha alisisitiza kuwa "Uangalifu wa mara kwa mara unahitaji kuoneshwa kwa utu na maendeleo fungamani ya watu madhubuti katika juhudi za kupambana na umaskini, kurejesha utu kwa waliotengwa na kutunza nyumba yetu ya pamoja (taz. Laudato Si’, 139)." Katika "mipango ya kukuza watu ni nzuri kwa kiwango ambacho inasaidiwa na mifumo ya kiuchumi inayojitegemea na ya muda mrefu, Papa amesema. Ni jambo la kupongezwa, basi, kwa sababu katika "uchanganuzi wao wa hali ya sasa, Jukwaa lao limepitisha dira ya kimataifa."

Juhudi na kutiwa moyo

Kuhusika kwa wazungumzaji wataalam kutoka tamaduni na dini mbalimbali, Papa alisema, "kunahimiza kuthamini na usikivu kwa mahitaji yote ya binadamu." Papa Francisko aliwatia moyo katika "juhudi zao, ambazo msingi wake ni kukiri utakatifu wa maisha ya mwanadamu na wamejitolea katika ujenzi wa ulimwengu uwe bora." Amewashukuru kwa kwa ujio wao na kuwabariki kwa kazi yao. Hatimaye aliwaomba wamkumbuke katika sala zao.

Papa na jukwaa la Uchumi
11 December 2024, 11:55