Papa Francisko na mzunguko mpya wa Katekesi:Jubilei 2025:Maria na wanawake 4 katika Biblia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Katekesi yake Baba Mtakatifu, Jumatano tarehe 18 Desemba 2024, akiwa katika Ukumbi wa Paulo VI alianza mzunguko mpya wa wa Jubilei 2025, kwa mada: " Yesu Kristo ni Tumaini letu," ambapo kipengele cha Kwanza kinahusu Utoto wa Yesu,unaopatikana katika kifungu cha Matayo kinachoeleza 'Ukoo wa Yesu' (Mt 1.1-17). Kuingia kwa Mwana wa Mungu katika historia. Somo la Injili lilisomwa kabla ya tafakari. "Ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka, Isaka alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yuda na ndugu zake, Yuda alimzaa Faresi na Zara kwa Tamari, [...] Salmoni alimzaa Boazi kwa Rakabu, Boazi alimzaa Obedi kwa Ruthu, Obedi alimzaa Yese, Yese alimzaa mfalme Daudi. Daudi alimzaa Sulemani kwa mwanamke aliyekuwa mke wa Uria [...]. Mathani akamzaa Yakobo, Yakobo akamzaa Yusufu, mume wa Maria, ambaye Yesu aitwaye Kristo alizaliwa kwake."
Baada ya somo hilo Papa Francisko alisema kusema: "Leo tunaanza mzunguko wa Katekesi utakaofanyika katika kipindi chote cha Mwaka wa Jubilei. Mada ya mzunguko huu wa katekesi ni "Yesu Kristo tumaini letu:" Yeye ndiye, kwa hakika, mwisho wa hija yetu na Yeye mwenyewe ndiye njia ya kufuata. Sehemu ya kwanza itashughulikia utoto wa Yesu, ambayo inasimuliwa kwetu na Wainjili Mathayo na Luka (rej. Mt 1–2; Luka 1–2). Injili za utoto wa Yesu zinaeleza juu ya ujauzito wa Yesu kwa bikira na kuzaliwa kwake kutoka tumboni mwa Maria; wanakumbuka unabii wa kimasiya ambao unatimizwa ndani Yake na kusema juu ya ukoo wa kisheria wa Yosefu, ambaye alipandikiza Mwana wa Mungu kwenye “shina” la ukoo wa Daudi. Tuliwakilishwa pamoja na Yesu kama mtoto mchanga, mtoto na Barubaru , mwenye kujitiisha kwa wazazi wake na, wakati huohuo, akijua kujiweka wakfu kikamili kwa Baba na Ufalme wake. Tofauti kati ya Wainjili hao wawili ni kwamba wakati Luka anasimulia matukio kupitia macho ya Maria, Mathayo anafanya hivyo kupitia yale ya Yoseph, akisisitiza juu ya ukoo huo ambao haujawahi kutokea."
Baba Mtakatifu alisema kuwa "Mathayo anafungua Injili yake na kanuni zote za Agano Jipya kwa “ukoo wa Yesu, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu” (Mt 1:1) kwa somo lililosomwa. Hii ni orodha ya majina ambayo tayari yapo katika Maandiko ya Kiebrania, ili kuonesha ukweli wa historia na ukweli wa maisha ya mwanadamu. Kwa hakika, ukoo wa Bwana unaundwa na historia ya kweli, ambapo kuna baadhi ya majina yenye matatizo ya kusema kidogo na dhambi ya Mfalme Daudi inapigiwa mstari (rej. Mt 1: 6)." Kwa njia hiyo kila kitu, hata hivyo, huisha na kusitawi ndani ya Maria na katika Kristo(taz. Mt 1:16”, na pia Barua ya kupyaishwa kwa Somo la historia ya Kanisa, 21 Novemba 2024). Papa alisema kuwa na kisha ukweli wa maisha ya mwanadamu unaonekana ambao unapita kutoka kizazi kimoja hadi kingine, ukijikita kwa mambo matatu: jina ambalo lina utambulisho na utume wa pekee; mali ya familia na watu; na hatimaye kushikamana kwa imani katika Mungu wa Israeli.
Ukoo ni aina ya fasihi, yaani, mtindo unaofaa kuwasilisha ujumbe muhimu sana: hakuna mtu anayetoa maisha yake peke yake, lakini anapokea kama zawadi kutoka kwa wengine; katika kesi hyoi, ni watu waliochaguliwa na ambao wanarithi amana ya urithi. Hata hivyo, tofauti na koo za Agano la Kale, ambapo majina ya kiume pekee ndiyo yanaonekana, ni kwa sababu katika Israeli baba ndiye anayempatia jina mtoto, na wanawake pia wanaonekana katika orodha ya Mathayo kati ya mababu wa Yesu. Hapo tunapata watano kati yao: Tamari, binti-mkwe wa Yuda ambaye, wakati mmoja alikuwa mjane, anajifanya kuwa kahaba ili kuhakikisha uzao kwa mumewe (rej Mwa 38); Rahabu, kahaba wa Yeriko anayeruhusu wapelelezi wa Kiyahudi kuingia katika nchi ya ahadi na kuiteka (rej.Yos 2); Ruthu, Mmoabiti ambaye, katika kitabu cha jina hilo hilo, anabaki mwaminifu kwa mama-mkwe wake, anamtunza na atakuwa nyanya wa Mfalme Daudi; Bath-sheba, ambaye Daudi alizini naye, na baada ya kuuawa mume wake, humzalisha Sulemani (rej 2 Sam 11); na hatimaye Maria wa Nazareti, mke wa Yoseph, wa ukoo wa Daudi: kutoka kwake Masiha, Yesu, alizaliwa.
Wanawake wanne wa kwanza hawakuunganishwa na ukweli wa kuwa wadhambi, kama inavyosemwa nyakati fulani, lakini kwa kuwa walikuwa wageni: wao ni wanawake wa kigeni kwa watu wa Israeli. Anachoeleza Mathayo ni kwamba, kama Benedikto wa kumi na sita alivyoandika, "kupitia kwao ulimwengu wa Mataifa unaingia ... katika ukoo wa Yesu-utume wake kwa Wayahudi na wapagani unaonekana" (The Childhood of Jesus, Milan - Vatican City 2012,15). Wakati wanawake wanne waliotangulia wametajwa pamoja na mwanamume aliyezaliwa kutoka kwao au yule aliyezaliwa na , Maria kwa upande mwingine, anapata umaarufu fulani, wakati huki anaashiria mwanzo mpya, yeye mwenyewe ni mwanzo mpya, kwa sababu katika hisotoria yeye si kiumbe binadamu tena mhusika mkuu wa kizazi, lakini ni Mungu mwenyewe.
Hili linaweza kuonekana wazi kutokana na kitenzi cha “anazaliwa" na kwamba: “Yakobo akamzaa Yusufu, mume wa Maria, ambaye Yesu aitwaye Kristo alizaliwa kwake” (Mt 1:16). Yesu ni mwana wa Daudi, aliyepandikizwa katika ukoo huo na Yoseph na aliyekusudiwa kuwa Masiha wa Israeli, lakini pia ni mwana wa Ibrahimu na wa wanawake wa kigeni, kwa hiyo amekusudiwa kuwa “Nuru ya Mataifa” (taz. Lk 2 :32) Mwana wa Mungu, aliyewekwa wakfu kwa Baba kwa utume wa kufunua uso wake (taz. Yh 1:18; Yh 14:9), anaingia ulimwenguni kama watoto wote wa wanadamu, kiasi kwamba huko Nazareti ataitwa: “mwana wa Yosefu" (Yh 6.42) au «mwana wa seremala” (Mt 13.55). Mungu wa kweli na mwanadamu wa kweli. Baba Mtakatifu Francisko kwa njia hiyo ameomba kuweka ndani yetu kumbukumbu za shukrani za mababu zetu. Na zaidi ya yote tunamshukuru Mungu, ambaye kwa njia ya Mama Kanisa, ametuzaa kwa uzima wa milele, uzima wa Yesu, tumaini letu, alihitimisha.