Papa Francisko:ukuzaji wa binadamu unahitaji uchumi endelevu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 11 Desemba 2024 alikutana na Shirika lisilo la Kiserikali, la kutoa Msaada wa wakimbizi na wahamiaji mjini Vatican. Akianza hotuba yake alisema kuwa "Ninayo furaha kuwakaribisha na kuwapongeza kwa hatua nzuri unayofanya kwa ajili ya wahamiaji wanaovuka Bahari ya Mediterania na wale wanaosafiri kwa njia ya Balkan. Asante! kiukweli, uokoaji wa wale ambao wana hatari ya kuzama katika boti mbaya, kama ukaribishaji wa kwanza wa wale wanaofika Ulaya mwishoni mwa safari ndefu na hatari za kila aina, ni kazi muhimu zaidi kuliko hapo awali. Hatua inayofuatwa na shirika lako inalenga kuokoa maisha ya binadamu: maisha ya watu wanaokimbia maeneo ambako mizozo mikubwa huzuka, ambayo mara nyingi huzua migogoro ya kibinadamu na pia kuhusisha ukiukaji wa haki za kimsingi za binadamu."
'Hawakutazama upande mwingine'
Papa amesema kuwa wao wanakabiliwa na mchezo mbaya wa wahamiaji wa kulazimishwa, ambayo kwa bahati mbaya wakati mwingine huwa janga, lakini wao hawajabaki bila kujali, lakini wamejiuliza: je mimi, sisi, tunaweza kufanya nini? Hawakutazama upande mwingine. Msingi wa mtazamo huu ni imani kwamba kila mwanadamu ni wa kipekee na utu wake hauvunjwa, bila kujali utaifa wake, rangi ya ngozi, maoni ya kisiasa au dini. Kwa bahati mbaya, mara nyingi hii haifanyiki na maisha mengi yananyonywa, kukataliwa, kunyanyaswa, kupunguzwa utumwa. Na kukabiliwa na ukubwa na utata wa jambo la uhamaji, mamlaka za kiraia haziwezi daima kukabiliana nalo kikamilifu kulingana na majukumu yao.
Pongezi kwa wanajoihusha kutoa muda wao
Kwa hiyo Papa amekaribisha hatua ya wale ambao hawaishi kwa kutazama mambo, kukosoa kutoka mbali, lakini wanahusika, wakitoa muda wao, taaluma zao na rasilimali zao ili kupunguza mateso ya wahamiaji, kuwaokoa, kuwakaribisha na kuunganisha. Mhamiaji lazima akaribishwe, asindikizwe,apewe hadhi na kuunganishwa. Ukarimu huo, bidii hiyo inawiana na Injili, inayotualika kutenda mema kwa kila mtu na kwa namna ya pekee kwa walio maskini zaidi na walioachwa zaidi, wagonjwa, watu walio hatarini. Baba Mtakatifu amehitimisha kwa kuwaomba waendelee hivyo na Mama maria awasaidia wahamiaji na awasadie wao katika Kazi yao. Amewabariki na kuwaomba tafadhali wasali kwa ajili yake.