Tafuta

2024.12.12 Papa na Uwakilishi wa Utume wa Kiinjili wa Yohane Mbatizaji kwa Warom nchini  Italia. 2024.12.12 Papa na Uwakilishi wa Utume wa Kiinjili wa Yohane Mbatizaji kwa Warom nchini Italia.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa Ujumbe wa Warom Italia:Hakuna anayeweza kututenganisha na upendo wa Mungu

Ushirikiano wa kidugu kati ya wakristo hasa ni ishara,ushuhuda,na chombo cha kwanza cha Uinjilishaji kwa ajili ya wema wa wote.Ni Hotuba ya Papa aliyokabidhi Uwakilishi wa Utume wa Yohane Mbatizaji kwa Warom nchini Italia,aliokutana nao tarehe 12 Desemba 2024 mjini Vatican.Papa anawapokea 'kama watoto wa Baba mmoja na Ndugu katika Kristo ambapo katika majeraha yake sisi sote tumepona,kama wasindikizaji katika hija ya imani na katika upendo na matumaini.'

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika hotuba ya Papa Francisko aliyokabidhi Uwakilishi wa Utume wa Yohane Mbatizaji wa Warom nchini Italia, aliokutana nao tarehe 12 Desemba 2024, mjini Vatican,anabainisha kuwa anawapokea kama "watoto wa Baba mmoja na Ndugu katika Kristo ambapo katika majeraha yake sisi sote tumepona, na kama wasindikizaji wa njia katika hija ya imani na katika upendo na matumaini.”

Hakuna awezaye kututengenisha na upendo wa Kristo

Papa amebainisha kuwa kwa kuwapokea kama wawakilishi wa Utume wa Kiinjili ya Yohane Mbatizaji nchini Italia, amependa kuwatumia salamu za kidugu  hata wajumbe wote wa watu wa Rom na ambao wanahudumia kila siku. Kwa pokea salamu hizi , Papa anapenda kupyaisha uhakika wa pamoja kwamba “ hakuna ambaye anaweza kututenganisha na upendo wa Mungu. Na uhakika huo unaweza kutufanya kuwa mashuhuda wanaoaminika kwa njia ya upendo hai, kwa njia ya baadhi ya uzoefu wa kushirikishana katika sala na huduma.”

'Umtumaini Bwana uwe hodari'

Papa Francisko aidha amesisitiza kuwa “Roho Mtakatifu anatuhuisha na kututuma kwa nguvu ya ujasiri na furaha ya kutangaza kwa pamoja Injili ya matumaini, kwa namna ya pekee ya Warom. Ushirikiano wa kidugu kati ya wakristo  hasa ni ishara, ushuhuda, na chombo cha kwanza cha Unjilishaji kwa ajili ya wema wa wote. Na kwa namna ya fumbo, umoja wa matendo ambao unauhishwa kutoka katika Injili unatukaribia kabisa katika umoja wa imani kwa njia ya utambuzi na kupongezana pamoja.” Papa Francisko anabainisha kuwa wakati tunajiandaa kuadhimisha Noeli Takatifu, hija yetu ya pamoja katika ardhi ambayo imejaa maneno ya mhubiri: “Umtumaini Bwana, uwe hodari, moyo wako uimarishwe na umtumaini Bwana” (Zab 27,14).  Papa amehitimisha akiwashukuru kwa moyo kwa hija yao. Anawakumbuka katika sala ya pamoja ambayo Yesu alitufundisha ya Baba Yetu.

Papa na Warom
12 December 2024, 11:07