Papa:Syria ni wakati nyeti katika historia yake,suluhisho la kisiasa litafutwe!
Angella Rwezaula – Vatican.
Utulivu, umoja, amani, usalama, urafiki, heshima kati ya dini mbalimbali, ndizo zawadi ambazo Baba Mtakatifu Francisko ameziomba kwa ajili ya Syria, nchi ambayo daima imekuwa ikifafanuliwa kama wakati wa kupendwa ambayo inakabiliwa na wakati tete katika historia yake baada ya kuanguka kwa utawala wa Bashar al Assad mikononi mwa waasi wa Hayat Tahrir al Sham ambao sasa wanaunda serikali ya mpito. Papa Francisko ameonesha hayo mara baada ya Katekesi yake, Jumatano tarehe 11 Desemba 2024 kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican.
Papa amesema “ Ninafuatilia kile kinachotokea Syria katika wakati huu mgumu katika historia yake. Natumaini kuwa suluhisho la kisiasa litafikiwa ambalo, bila mizozo na migawanyiko zaidi, litahamaisha uthabiti na umoja wa nchi kwa uwajibikaji. Ninaomba kwa maombezi ya Bikira Maria kwamba watu wa Syria wapate amani na usalama katika nchi yao waipendayo na kwamba dini mbalimbali ziweze kutembea pamoja kwa urafiki na kuheshimiana kwa manufaa ya taifa hilo lililoteswa na miaka mingi ya vita.”
Salaamu mbali mbali
Baba Mtakatifu Francisko aidha alitoa salamu kwa mahujaji kutoka pande za dunia. Na kwa upande wa Mahuhaji wa kiitaliano alisema “Ninawakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano. Hasa, ninawasalimu wawakilishi wa Muungano wa Folkloric wa Kiitaliano katika maadhimisho ya miaka 40 ya shughuli na kuwahimiza kuhifadhi urithi wa kitamaduni wa eneo hilo lenye thamani nyingi za kidini na kiroho; Kisha nisalimie Wajumbe wa Jimbo la Latina ambao wanaadhimisha miaka 90 tangu kuanzishwa kwake wa Foundation na ninamwomba Bwana atie moyo miradi na mipango yake kwa manufaa ya watu wote.
“Ninawakaribisha kwa moyo mkunjufu wazima moto wanaotoka Chieti na ninachukua fursa hii kuwaeleza wao na wenzao wote shukrani zangu kwa kile mnachowakilisha na kwa kile mnachofanya kwa ajili ya jamii, katika huduma za kila siku na katika dharura kuu.” Hatimaye, mawazo yangu yanawaendea vijana, wagonjwa, wazee na wenye ndoa wapya. Katika wakati huu wa Majilio, muendelee kwa moyo wa ujasiri kumwelekea Bwana anayekuja kwa ajili ya wokovu wetu,” Papa alisema.
Maombi kwa ajili ya Ukraine
Na mimi ninafikiria kila wakati juu ya Ukraine inayoteswa ambayo inateseka sana kutokana na vita hivi. Tuombe kwamba njia ya kutokea ipatikane. Na ninafikiria Palestina, Israel, Myanmar. Amani irudi, iwe na amani! Vita daima ni kushindwa. Tunaomba amani.”