Watawa Wakarmeli peku wa Compiègne,waliokatwa vichwa 1794 watakuwa watakatifu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Wakati wa Mkutano uliofanyika Jumatano tarehe 18 Desemba 2024 kati ya Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza Watakatifu, Baba Mtakatifu Mkuu aliidhinisha kura za upendeleo za Kikao cha Kawaida cha Makardinali na Maaskofu na Wajumbe wa Kanisa, na kuamua kueneza kwa Kanisa zima la Ulimwengu juu ya ibada ya Mwenyeheri Teresa wa Mtakatifu Agustino (Jina la ubatizo Maria Maddalena Claudia Lidoine) na wenzake 15 wa Shirika la Watawa Wakarmeli peku wa Compiègne, nchini Ufaransa, wafiadini ambao waliouawa kwa sababu ya kuchukiwa Imani yao mnamo tarehe 17 Julai 1794, huko Paris(Ufaransa), na kuwaandikisha katika orodha ya Watakatifu (Sawa ya kutangazwa kuwa Watakaifu).
Kifo cha kishahidi cha Eduardo
Na wakati wa kikao hicho, Baba Mtakatifu pia aliidhinisha Baraza la Kipapa la mchakato wa Kuwatangaza watakatifu kuhusu Amri inayohusu hawa wafuata: - kifo cha kishahidi cha Mtumishi wa Mungu Eduardo Profittlich, wa Shirika la Yesu, (Mjesuit) aliyeikuwa Askofu Mkuu wa Adrianople, Msimamizi wa Kitume wa Estonia; alizaliwa tarehe 11 Septemba 1890 huko Birresdorf (Ujerumani) na alikufa tarehe 22 Februari 1942 mwanafunzi wa samani wa gereza huko Kirov (Urusi);
-Kifo cha kishahidi cha Mtumishi wa Mungu Elia Comini, aliyekuwa Padre wa Shirika la Mtakatifu Francis de Sales, aliyezaliwa huko Calvenzano ya Vergato (Italia) tarehe 7 Mei 1910 na kuuawa kwa chuku ya Imani mnamo tarehe 1 Oktoba 1944 huko Pioppe ya Salvaro (Italia) );
-fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Áron Márton, Askofu wa Alba Iulia, aliyezaliwa tarehe 28 Agosti 1896 huko Csíkszentdomokos (sasa ni Romania) na kufariki tarehe 29 Septemba 1980 huko Alba Iulia (Romania);
-Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Giuseppe Maria Leone, aliyekuwa Padre wa Shirika la Mkombozi Mtakatifu zaidi, aliyezaliwa tarehe 23 Mei 1829 huko Casaltrinità (sasa Trinitapoli, Italia) na kufariki huko Angri (Italia) tarehe 9 Agosti 1902;
-Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Peter Goursat, Mleu mwaminifu, aliyezaliwa tarehe 15 Agosti 1914 huko Paris (Ufaransa) na kufariki tarehe 25 Machi 1991.