Tafuta

2023.06.06 Kitabu cha Joaquín Navarro-Valls: "Miaka yangu na Yohane Paulo II" . 2023.06.06 Kitabu cha Joaquín Navarro-Valls: "Miaka yangu na Yohane Paulo II" . 

Kard.Parolin:Navarro-Valls alikuwa mtu wa ubinadamu mkubwa na kiroho

Kitabu chenye kichwa:’Miaka yangu na Yohane Paulo II,Maelezo Binafsi’ kimewasilishwa,Juni 5,katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu.Katika ujumbe wa Kardinali Parolin ameelezea juu ya ubora wa kumbukumbu hizo kwamba pia zina mafundisho ya wakati mgumu wa kihistoria tunaoishi.Kinachojitokeza ni ukurasa wa maisha ya kidunia ya Kanisa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Joaquín Navarro-Valls alikuwa mtu wa ubinadamu mkubwa na kina mashuhuri wa kiroho, mtaalamu aliyejaliwa sifa za kipekee, mzungumzaji hodari na anayethaminiwa. Huo  ni wasifu wa Navarro-Valls, aliyewahi kuwa Msemaji wa  Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican  kati ya mwaka 1984 na 2006, kwa mujibu wa  Katibu wa Vatican Pietro Parolin wakati wa kuwasilisha mada, Jumatatu tarehe 5 Juni 2023 kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu (Santa Croce) kwa ajili ya toleo la kitabu kwa lugha ya Kiitaliano chenye kichwa:  Miaka yangu na Yohane Paulo II - Maelezo ya kibinafsi”

Katika ujumbe wa Katibu wa Vatican  uliosomwa na mkuu wa chuo kikuu, Padre Luis Navarro, anaadika kuwa  kumbukumbu ya Navarro-Valls ambaye alijipambanua kwa kujitolea kwake makao makuu matakatifu na zaidi ya yote, kwa uhusiano wa uelewa wa kina pamoja na Yohane Paulo II, akiandamana naye, kwa kujikana nafsi, katika nyakati za furaha na mateso ya huduma ya Mtume Petro. Tukio hili linafaa zaidi kuelezea kumbukumbu ya kujitolea na ya shukrani ya Mtakatifu Yohane Paulo II, ambaye alikuwa na mmoja wa washirika wake wa karibu na waaminifu kwa marehemu Navarro-Valls, aliandika Kardinali Parolin katika ujumbe huo. “Nina hakika kwamba kusoma maelezo haya ya kibinafsi si tu kwamba kutatuwezesha kufahamu vipengele ambavyo havijachapishwa vya matukio ya kihistoria kuhusu Kanisa na maisha ya Papa mpendwa wa Poland, lakini pia kuingia kikamilifu zaidi katika hali yake ya kiroho na utakatifu. Na kwa hakika, aliongeza, mvuto kwa dhamiri za watu, kukimbilia sala na ujasiri wa kitume ambao” Yohane Paulo wa Pili alikabiliana nao hali zisizostarehesha na ngumu hujitokeza.

Katibu wa Vatican pia alipendekeza jinsi ya kuteka kutoka kwa kitabu mafundisho kwa wakati mgumu wa kihistoria tunaoishi, kufurahiya ukurasa wa maisha ya kidunia ya Kanisa, hata katika nyanja zake za kila siku na za kibinafsi. Jedwali la pande zote la uwasilishaji wa kitabu  lililosimamiwa na mwandishi wa habari Valentina Alazraki - lilihudhuriwa na: Diego Contreras, mhariri wa kitabu  pamoja na maprofesa wa Kitivo cha Mawasiliano cha Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu; Giovanni Grasso mshauri kwa vyombo vya habari na mawasiliano ya Urais wa Jamhuri ya Italia; Padre Federico Lombardi, rais wa Mfuko wa Joseph Ratzinger-Benedict XVI na mrithi wa Navarro-Valls kama Msemaji mkuu wa Vyombo vya habari Vatican; Lina Petri, mfanyakazi wa Ofisi ya Vyombo vya Habari tangu mwaka 1986, mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Mfuko wa  Yohane Paulo I Vatican; Francesco Rutelli, meya wa zamani wa Roma kati ya 1993 na 2001.

Kitabu kilichochapishwa nchini Uhispania na Tahariri ya Sayari yenye kichwa “Mis años con Juan Pablo II”  na kuwasilishwa huko Madrid mnamo tarehe 24 Mei kwa kuingilia kati kwa Alessandro Gisotti, Naibu mkurugenzi wa wahariri wa vyombo vya habari vya Vatican kinakusanya maandishi ya kibinafsi ya Navarro- Valls ambaye anasimulia huduma yake ya moja kwa moja kwa Papa. Hizi ni kurasa ambazo, zilizoandikwa kwa namna ya shajara na kuchapishwa kwa amri ya mwandishi tu mara baada ya kifo chake mnamo tarehe 5 Julai 2017, akiwa na umri wa miaka 80, ambazo zinatoa hali ya  kuvutia sehemu yake ya juhudi za Vatican  na kwa msuko suko  mgumu wa mambo ya sasa ya kimataifa na mhariri wa kitabu pia anafichua maelezo ya thamani ya maisha ya kila siku ya Yohane Paulo II.

Kitabu kuhusu ushuhuda wa Navarro na Papa Yohane Paulo II
06 June 2023, 15:08