Tafuta

Matukio ya Ufunguzi wa Jubilei Matukio ya Ufunguzi wa Jubilei 

Jubilei:Audio,video,podcast vinapatikana katika Vyombo vya habari,Vatican ili kuishi matukio mbashara!

Katika tovuti ya Habari za Vatican zenye lugha 53,ikijumuisha na lugha ya ishara,shukrani kwa mikondo ya sauti ya Radio Vatican,video za Vyombo vya Habari vya Vatican na ushirikiano na YouTube,kila mwamini ataweza kuhudhuria matukio ya Jubilei.Maudhui yote yaliundwa ili kuunda daraja kati ya ulimwengu wa kidijitali na mwelekeo wa kiroho.Usikose kushiriki hata wasioweza kufika Roma.

Vatican News.

Tarehe 24 Desemba 2024 katika mkesha wa Noeli,Baba Mtakatifu Francisko  atafungua wazi Mlango Mtakatifu uonaashiria kuanza kwa Jubilei ya Matumaini. Katika tukio hilo, Papa Francisko anatualika kusali na kujiandaa  mwaka mzima, “kwa sababu  Jubilei hiyo inatutia nguvu ya imani, kwa kutusaidia kutambua Kristo Mfufuka kwa njia ya maisha yetu, na kutubadili kuwa wahahija wa matumaini” (Maneno ya Papa katika nia za maombi kwa mwezi Desemba 2024). Tukio hili la Kanisa zima la Ulimwenguni linaweza kushuhudiwa na kushirikishwa na kila mtu, pia kutokana na makubaliano na watangazaji, magazeti na majukwaa ya mtandao kijamii kutoka sehemu zote za dunia, na Vyombo vya Habari vya Vatican (Vatican Radio-Vatican News, Osservatore Romano, Vatican Media).

Shiriki katika wakati halisi

Na hasa, katika tovuti ya Vatican News, ambayo(mfumo wake  unajumuisha lugha 53, ikiwa ni pamoja na lugha ya ishara), itaruhusu kila mwamini, shukrani kwa mikondo ya sauti ya Radio Vatican, video za Vatican Media na ushirikiano na YouTube, kuhudhuria matukio yote ya Jubilei na ya Kipapa. Kupitia ufunikaji kamili na unaoweza kufikiwa, itawezekana kushiriki, kwa wakati halisi na kwa mahitaji, katika matukio makuu ya Jubilei ya 2025, kwa kujikita katika safari ya kweli ya kiroho iliyoboreshwa na vipengele vya habari, vya kiutamaduni na vya kihistoria.

Pendekezo pana

Kuanzia kufunguliwa kwa Milango Makatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro hadi mwisho wa Mwaka Mtakatifu, toleo la Habari za Vatican kwenye YouTube litakuwa tofauti na la kuvutia. Utiririshaji wa moja kwa moja utaruhusu mamilioni ya waamini kujiunga katika maombi, kutazama picha za ubora wa hali ya juu, na maoni na habari katika lugha tofauti, ikiwa ni pamoja na lugha ya ishara.

Kando na matangazo ya moja kwa moja(mbashara)ya Vatican News,  kwenye YouTube itatoa maudhui mbalimbali ya vyombo vya habari yaliyoundwa kukidhi mahitaji ya kila aina ya hadhira kama vile:

• Video fupi ambazo zitaeleza matukio muhimu na ya kusisimua zaidi ya Jubilei katika umbo la haraka na la kuvutia, linalofaa kushirikishwa na kugundua kwa urahisi.

• Mahojiano ya kina ya kipekee na mashuhuda na wahusika wakuu wa maisha ya kikanisa na kiutamaduni, ili kutafakari maana ya Jubilei na umuhimu wake wa kiroho katika jamii ya kisasa.

• Vodcast na podcast: maudhui ya sauti na video yaliyoundwa kusindikizana na watazamaji katika kugundua mada kuu za Mwaka Mtakatifu, kutoa chakula cha kiroho, mawazo, historia za imani na ushuhuda wa mahujaji kutoka ulimwenguni kote

Ukaribu wa kiroho kwa wale ambao hataweza kufika Roma

Mchakato huu wa Vyombo vya habari (unaoweza kufikiwa pia kwa sauti kupitia programu ya Radio Vatican na kwa video kupitia programu ya Habari za Vatican, pamoja na kutoa ukaribu wa kiroho kwa wale ambao hawawezi kufika Roma, itakuwa fursa ya kugundua upya dini, historia na utamaduni unaohusishwa na Jubilei na Kanisa zima. Kwa njia hiyo kila maudhui yataundwa ili kuunda daraja kati ya ulimwengu wa kidijitali na mwelekeo wa kiroho, na kuwapa waamini na wale wanaopenda kuhisi kama sehemu hai ya tukio ambalo lina mizizi ya kina katika utamaduni wa Kikristo. Kwa upande wa Vatican News, shukrani pia kwa YouTube, itaweza kutoa uzoefu unaoweza kufikiwa na wote, ikisindikizana na kila mtu katika safari hii ya imani, matumaini na ushirika wa wote ulimwenguni.

FUATILIA JUBILEIO 2025
23 December 2024, 10:14