Kuna ukosefu wa uhuru wa kidini nchini Nicaragua Kuna ukosefu wa uhuru wa kidini nchini Nicaragua  (AFP or licensors)

Nicaragua:Padre mmoja amekamatwa baada ya Misa ya mwisho wa mwaka

Huyu ni Padre Gustavo Sandino,Paroko wa Jimbo la Jinotega.Katika siku za hivi karibuni mapadre wasiopungua 14,waseminari wawili na Askofu wamekamatwa.Kardinali Brenes alionesha ukaribu wake kwa familia na jumuiya za mapadre.Katika baadhi ya makanisa Misa zilizopangwa hazikufanyika na waamini walialikwa kurudi nyumbani.

Vatican News

Padre Gustavo Sandino, Paroko wa Parokia ya Mama Yetu wa Huzuni, alikamatwa tarehe 31 Desemba 2023 baada ya kuadhimishwa Misa ya Dominika huko Mtakatifu  María wa Pastasma, Jimbo katoliki la Jinotega, Nicaragua. Vyanzo vya habari viliripoti hilo na wakili aliye uhamishoni Martha Patricia Molina pia alithibitisha hilo. Huko Managua, hata hivyo, Padre Fernando Téllez Báez, paroko wa Parokia ya Mama yetu wa Amerika, alichukuliwa mapema asubuhi ya tarehe 31 Desemba na Padre Jader Hernández, parokia ya Mama wa Mchungaji wa Mungu, majira ya jioni ya tarehe 30 Desemba 2023. Katika siku za hivi karibuni, hata hivyo mapadre wasiopungua 14 wamekamatwa, wakiwemo waseminari wawili: Alester Saenz na Tony Askofu Rolando José Álvarez Lagos, wa Matagalpa na msimamizi wa kitume wa Kanisa hilo la Jimbo ya Estelí, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 26 jela bila kufuata utaratibu wa kisheria.


Tarehe 31 Desemba 2023, Kadinali Leopoldo José Brenes Solórzano, na askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Managua, wakati wa Misa katika Kanisa Kuu alionesha ukaribu wake “kwa familia na jumuiya ambazo kwa wakati huu zinakosa mapadre wao” akiwaalika kila mtu kubakikwa nguvu ya  umoja katika sala. “Umoja wa kikanisa ni nguvu zetu. Pamoja na Maria, mama yetu, chini ya msalaba - Bwana atufariji na kutuonesha huruma yake.” Alihitimisha Kardinali Brenes. Wakati huo huo, wakili Molina alisema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa amepata habari kuwa tarehe 31 Desemba katika baadhi ya makanisa Misa iliyopangwa haikuadhimishwa na waamini kualikwa kurejea nyumbani. Haijulikani, kwa sasa, ikiwa mapadre wa parokia hizi wametekwa nyara.


Kufikia sasa si serikali wala polisi ambao wamethibitisha au kukana kukamatwa kwa mapadre  hao. Wawakilishi wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu walisema kwamba Nicaragua inakwenda “kuongezeka” kutoka katika utawala wa sheria na “uhuru wa kimsingi” kwa kuwatesa“viongozi wa kisiasa na wazawa, washiriki wa Kanisa Katoliki, wanaharakati na waandishi wa habari” kwa “mara kwa mara ambapo  kesi za kuwekwa kizuizini kiholela zinajionesha.”

Kanisa la Nicaragua linateswa kunyimwa uhuru Maaskofu na Mapadre
01 January 2024, 15:50