2024.12.09 Papa alikutana na washiriki wa Kiongamano la Kimataifa la Taalimungu. 2024.12.09 Papa alikutana na washiriki wa Kiongamano la Kimataifa la Taalimungu.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa Wataalimungu:Ukamilifu wa taalimungu unaundwa na wanaume na wanawake!

Papa Francisko akikutana na washiriki wa Kongamano la Kimataifa kuhusu mustakabali wa Taalimungu,lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu,alitoa hotuba yake huku kuonesha nuru inayoleta Injili ili iweze kufikiwa na wote na kusaidia kufikiri upya katika ulimwengu tata.Papa anatuhimiza kupinga itikadi ambazo husawazisha kila kitu na kuua ukweli,mawazo na jamii.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 9 Desemba 2024 alikutana na  washiriki wa Kongamano la Kimataifa kuhusu ‘mustakabali wa Taalimungu’ lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. Katika hotuba yake alifurahi kuwaona na kujua kwamba idadi kubwa kama hii ya maprofesa, watafiti na wakuu kutoka ulimwenguni kote  wamekusanyika ili kutafakari jinsi gani inayofaa kurithi   urithi mkuu wa kitaalimungu wa vizazi vilivyopita na kufikiria mustakabali wake. Papa alishukuru Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu kwa mpango huo. Na kuwashukuru pia wataalimungu, kwa kazi yao, ambayo mara nyingi imefichika lakini ni ya muhimu sana. Ni matumaini yake kwamba Kongamano hilo litaashiria hatua ya kwanza ya ubia wenye manufaa wa pamoja. Papa alieleza alivyambiwa kwamba baadhi  ya taasisi za kitaaluma, vyama vya kitaalimungu na baadhi yao kama watu binafsi wamechangia gharama za usafiri za wengine kwa namna fulani na kwa hiyo amewasifu kuwa. Hii ni nzuri sana! Na wasonge mbele pamoja! Alibainisha jinsi hatua hiyo ya upendo imewezesha hata kujitoa kifedha, ni nzuri. Kwa sababu upendo unaposimama kuna kitu kinakosekana.

Taalimungu imezaliwa na urafiki na Kristo

Papa alipofikiria Taalimungu nuru ilimjia akilini. Shukrani kwa nuru, vitu vinatoka gizani, nyuso zinaonesha msingi wao, maumbo na rangi za ulimwengu hatimaye huonekana. Nuru ni nzuri kwa sababu hufanya vitu vionekane lakini bila kujionesha. Je, yeyote kati yao amekwisha mwanga? Walijibu kuwa ‘Hapana,’ lakini tunaona kile ambacho mwanga hufanya yaani vitu vionekane, kila mmoja, lakini lakini bila kuona mwanga, kwa sababu ni busara, upole, unyenyekevu na, kwa hiyo, bado hauonekani. Nuru ni "fadhili." Taalimungu pia iko hivyo: inafanya kazi kwa utulivu na unyenyekevu ili nuru ya Kristo na Injili yake iweze kujitokeza. Uchunguzi huu unaweza kukuelekeza njia. Kutafuta neema ya Mungu na kudumu katika neema ya urafiki na Kristo, nuru ya kweli iliyokuja katika ulimwengu huu. Taalimungu yote imezaliwa na urafiki na Kristo na upendo kwa kaka na dada zake na ulimwengu wake: ulimwengu huu, mara moja wa ajabu na wa kusikitisha, uliojaa uzuri wa ajabu lakini pia mateso makubwa. Papa Francisko alieleza  jinsi ambavyo wengine kwa  siku hizi watakuwa wanafanya kazi pamoja juu ya "wapi", "vipi" na "kwa nini" ya Taalimungu. Tunaweza kujiuliza: Taalimungu, iko wapi? inakwenda na nani? Inafanya nini kwa ubinadamu?

Taalimungu ifanyike kwa wote

Katika siku hizi za mafunzo yao zitathibitisha kuwa muhimu kwa kushughulikia masuala haya na kuhoji ikiwa urithi wa kitaalimungu wa zamani bado unaweza kuzungumza na changamoto za leo na kutusaidia kufikiria siku zijazo. Hii ni safari ambayo wameitwa kufanya pamoja kama wataalimungu wa jinsia zote mbili. Hapo Papa alifikiria kipindi katika Kitabu cha Pili cha Wafalme. Wakati wa kurejeshwa kwa Hekalu huko Yerusalemu, kifungu kilikuja kujulikana; labda lilikuwa toleo la kwanza la Kumbukumbu la Torati, ambalo lilikuwa limepotea. Kuhani na wasomi kadhaa walikisoma, kama vile mfalme. Walihisi umuhimu wake lakini hawakuielewa. Kwa hiyo mfalme aliamua kumpatia mwanamke, Hulda, ambaye mara moja alielewa maana yake na alisaidia kundi la wanazuoni, wanaume wote - kuifahamu (Taz. 2 Wafalme 22:14-20). Kuna mambo ambayo ni wanawake pekee wanayaelewa na taalimungu inahitaji mchango wao. Taalimungu ya wanaume wote ni taalimungu isiyokamilika. Bado tuna safari ndefu katika mwelekeo huu.

Dawa dhidi ya kurahisha mambo ni 'Furaha ya Ukweli'

Jambo la kwanza la kufanya, katika kufikiria upya jinsi ya kufikiria, ni kusonga zaidi ya kurahisisha. Ukweli ni tata; changamoto ni mbalimbali; historia imejaa uzuri na wakati huo huo kuharibiwa na uovu. Wakati mtu hawezi au hataki kukabiliana na utata wake wa kushangaza, basi yeye huwa rahisi kurahisisha. Kurahisisha, hata hivyo, kunaharibu ukweli; kunaleta mawazo matupu na ya upande mmoja na kunazalisha ubaguzi na mgawanyiko. Hiyo, kwa mfano, ndivyo hasa itikadi hufanya. Itikadi ni kurahisisha ambayo inaua: inaua ukweli, inaua mawazo, inaua jamii. Itikadi husawazisha ukweli kwa wazo moja lisilo na kina, ambalo - kama kasuku ambaye kisha hurudia kwa umakini na kuendesha. Dawa moja ya kurahisisha inaoneshwa na Katiba ya Kitume Veritatis Gaudium: njia za kinidhamu na mtambuka (Foreward, 4c). Hii inahusisha kuruhusu tafakari ya kiaalimu kuchachuliwa pamoja na taaluma nyingine kama vile: falsafa, fasihi, sanaa, hisabati, fizikia, historia, sheria, siasa na uchumi. Mafundisho haya yanapaswa kuchachua, kwa sababu, kama vile hisia za mwili, kila moja ina kazi yake maalum, lakini zinahitajiana, kwa maana, kama mtume Paulo anavyoonesha, “Kama mwili wote ungekuwa jicho, kusikia kungekuwa wapi? Ikiwa mwili wote ungesikia, hisia ya kunusa ingekuwa wapi?" (1Kor 12:17).

Miaka 750 ya wataalimungu wakuu:Thomas na Bonaventure

Mwaka huu tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 750 ya kifo cha wataalimungu wawili wakuu: Mtakatifu Thomas Aquinas na Mtakatifu Bonaventure. Thomas anatuambia kwamba hatuna hisia moja, lakini hisia nyingi na tofauti ili ukweli tusiuepuke (De Anima, lib. 2, lect. 25). Na Bonaventure anasema kwamba kwa kiwango ambacho mtu “anamwamini, kumtumaini na kumpenda Yesu Kristo” mtu huyo “anapata tena kusikia na kuona..., kunusa..., kuonja na kugusa”(Itinerarium Mentis in Deum, IV, 3). Kwa kusaidia kutafakari upya jinsi ya kufikiri, taaalimungu itang'aa tena inavyostahili, katika Kanisa na katika tamaduni mbalimbali, ikisaidia kila mmoja katika kutafuta ukweli. Hiyo ndiyo shauku. Papa alipenda kuwapa mwaliko kwamba Taalimungu ipatikane na wote. Kwa muda sasa, katika sehemu nyingi za dunia kumekuwa na shauku miongoni mwa watu wazima kuanza tena elimu yao, kutia ndani mafunzo yao ya kitaaluma. Wanaume na wanawake, hasa katika umri wa kati na labda tayari wana shahada, hamu ya kuimarisha imani yao, kujaribu kitu kipya; mara nyingi hujiunga na kozi za chuo kikuu.

Watu hata wa umri wa kati wanatamani kusoma taalimungu

Hili ni jambo linalokua na linafaa maslahi kwa upande wa jamii na Kanisa. Umri wa kati ni wakati maalum katika maisha. Ni wakati ambapo mtu hufurahia usalama fulani wa kitaaluma na utulivu wa kihisia, lakini pia wakati ambapo kushindwa huhisiwa kwa uchungu na maswali mapya hutokea kama ndoto za ujana zinavyofifia. Hili linapotokea, watu wanaweza kuhisi wameachwa au hata katika hali ngumu - mgogoro wa katikati ya maisha. Kisha wanahisi hitaji la kufanya upya azma yao, hata hivyo kwa kujaribu, labda hata kwa msaada. Taalimungu inaweza kuwa mwongozo huo katika safari! Papa Francisko amewaomba  ikiwa mtu yeyote wa watu hawa atabisha hodi kwenye mlango wa taalimungu, wa shule za taalimungu,wapate kufunguliwa. Aidha wahakikishe kwamba wanawake na wanaume hawa wanapata katika taalimungu  nyumba ya wazi, mahali ambapo wanaweza kuanza tena safari yao, mahali ambapo wanaweza kutafuta, kupata na kutafuta tena. Kwa njia hiyo wataalimungu hao, Papa amekazia akiwaomba wawe tayari kwa hilo. Wafanye marekebisho ya kimawazo kwa programu zao za masomo ili taalimungu iweze kupatikana kwa wote.

Mkutano wa kushirikishana wote

Papa Francisko alielezwa kwamba katika mkutano huo hawatakuwa  na mkutano ambao mwingine au watu wachache watazungumza na wengine kusikiliza (au kulala hata usingizi!), badala yake kila mtu atapata nafasi ya kuzungumza na kusikilizwa. Alisifu kwamba  ni nzuri kwa sababu kila mtu ana kitu cha kutufundisha. Hata wanawake, wazee, watoto na wenye busara. Papa Francisko aliliomba Baraza la Kipapa la  Utamaduni na Elimu wamfahamishe matokeo ya mijadala yao ambayo itakuwa tayari na alitanguliza shukrani. Kwa kuhitimisha alitoa baraka yake kutoka moyoni na kuwaomba tafadhali wamwombee na yeye. Na kwamba kazi hii ni ya kufurahisha, lakini ni ngumu!

Papa na wataalimungu

 

09 December 2024, 16:17