Papa anakutana na Macron:'Asante kwa ishara ya kuja hapa'
Salvatore Cernuzio – Vatican
“Ninakushukuru kwa ishara hii ya kuja hapa. Ishara hii inaonesha utu wako, ukitafuta mkutano. Asante sana kwa muda wako." Papa Francisko alikaribishwa na Rais wa Ufaransa Bwana Emmanuel Macron kwa maneno ya shukrani, aliyefika Ajaccio kumuaga muda mfupi kabla ya kuondoka Corsica, kuja Roma ikiwa ni katika Ziara yake ya kitume ya 47, ambapo amefika huko katika fursa ya Kongamano kuhusu "Udini Maarufu wa watu wa Mungu katika Mediteranea."
Kitabu kuhusu Notre-Dame kama zawadi
Katika chumba kidogo kwenye Uwanja wa ndege uliopewa jina la Napoleon, aliyezaliwa katika kisiwa hicho, chumba kilichowekwa kiti cha mkono chenye koti la Papa na bendera za Jiji la Vatican, Ufaransa na Ulaya, Papa na rais waliingia pamoja kupitia lango moja kabla ya saa kumi na mbili jioni na wajumbe wao husika. Rais Macron, kama ilivyokuwa zamani katika vikao vya Vatican, au katika mikutano ya Marseille mnamo 2023 au G7, aliweka ishara za upendo kwa Papa. Mara moja alimkabidhi zawadi yake ambayo ni kitabu kikubwa kilichotolewa kwa Kanisa Kuu la Notre-Dame, (Mama Yetu la Paris) lililokarabatiwa baada ya kuungua moto mkali mnamo 2019 na kufunguliwa tena kwa umma Juma moja lililopita, tarehe 7 Desemba 2024. Mkuu wa nchi alipitia baadhi ya kurasa za kitabu hicho.
Usipoteze hali yako nzuri
Papa alijibu zawadi hiyo kwa medali za upapa na hati za majisterio. Hasa, Papa Fransisko alichukua nakala ya Evangelii Gaudium kutafuta ukurasa unaotaja pendekezo la Mtakatifu Thomas More - ambalo alirudia mara kwa mara katika hotuba zake – la kutopoteza ucheshi mzuri. Papa alielekeza jambo hilo kwa Macron kumtaka asome, rais akajibu kwa tabasamu na kumpa mkono Papa.
Asante kwa ziara yako
Wakiwa wameketi kwenye viti, wawili hao walipeana mikono na kiongozi wa Ufaransa akamshukuru Papa kwa ziara yake, huku akisisitiza kwamba ameona furaha ya watu wa Corsica, "amejivunia sana" kwa kuweza kumkaribisha Papa. Rais Macron alimshukuru Jorge Mario Bergoglio "kwa niaba ya Corsica na Ufaransa"; pamoja na hayo, mateso kutokana na kimbunga katika visiwa vya Ufaransa vya Mayotte vilivyosababisha mamia ya wahanga, kukumbukwa leo hii na Papa katika sala ya Malaika wa Bwana. Kutoka hapo, mazungumzo nyuma ya milango iliyofungwa, kitendo cha mwisho kabla ya sherehe ya kuaga katika uwanja wa ndege mwishoni mwa safari ya haraka ambayo iliashiria sura mpya katika historia kwa kisiwa cha Mediterania.