2024.12.07 Papa apokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa:India,Jordan,Denmark,Luxembourg,São Tomé na Principe,Rwanda,Turkmenistan,Algeria,Bangladesh,Zimbabwe na Kenya. 2024.12.07 Papa apokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa:India,Jordan,Denmark,Luxembourg,São Tomé na Principe,Rwanda,Turkmenistan,Algeria,Bangladesh,Zimbabwe na Kenya.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa apokea hati za utambulisho wa mabalozi wasio wakazi kuwakilisha nchi zao mjini Vatican

Ulimwengu wetu unazidi kukumbwa na matatizo yanayoathiri familia nzima ya kibinadamu na ni wito wa kuchukuliwa hatua kwa pamoja na wote wanaohangaikia wakati ujao wa sayari yetu.Ni Maneno ya Papa alipokutana na Mabalozi wapya wasio na makazi wakati wa kuwakilisha hati za utambulisho kwa Papa.Papa alifikiria juu ya athari mbaya zinazoendelea za mabadiliko ya tabianchi,ambazo huathiri mataifa yanayoendelea na wanajamii maskini na migogoro ya silaha ambayo husababi madhara ya binadamu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 7 Novemba 2024 amekutana na baadhi ya Mabalozi wasio na makazi ambao waliwakilisha Hati za Utambulisho, kutoka India, Jordan, Denmark, Luxembourg, São Tomé na  Principe, Rwanda, Turkmenistan, Algeria, Bangladesh, Zimbabwe na Kenya kuwakilisha nchi zao mjini Vatican. Katika hotuba yake Papa amewakaribisha wote na kwamba  wawafikishie  salamu zake  za heshima kwa Wakuu wa Nchi zao,pamoja na uhakika wa maombi yake kwa ajili yao. Kama wanavyofahamu vyema, wanaanza majukumu yao mapya katika wakati muhimu wa diplomasia ya kimataifa. Ulimwengu wetu unazidi kukumbwa na matatizo yanayoathiri familia nzima ya kibinadamu na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua kwa pamoja na wote wanaohangaikia wakati ujao wa sayari yetu. Katika hilo Papa amefikiria juu ya athari mbaya zinazoendelea za mabadiliko ya tabianchi, ambayo huathiri sana mataifa yanayoendelea na wanajamii maskini zaidi, migogoro ya silaha ambayo husababisha mateso mengi kwa kaka na dada zetu wengi, na hali mbaya ya wahamiaji na wakimbizi wengi wanaokimbia nchi zao katika kutafuta maisha bora ya baadaye ya familia zao.

Papa apokea hati za Utambullisho kutoka kwa baadhi ya mabalozi wasio wakazi
Papa apokea hati za Utambullisho kutoka kwa baadhi ya mabalozi wasio wakazi

Papa alisema kuwa “Masuala hayo hayana suluhishi rahisi, wala hayawezi kutatuliwa kwa matendo ya taifa moja au kundi dogo la mataifa. Kila nchi lazima iwe na sauti katika kushughulikia matatizo haya ya kimataifa na kutayarisha ufumbuzi wa kina na wa muda mrefu. Katika suala hili, kazi ya subira ya diplomasia ni ya umuhimu mkubwa. Huku kukiwa na matatizo, vikwazo, mgongano wa silaha na madai yanayokinzana ya kuwa upande wa haki, jumuiya ya kimataifa haiwezi kukataa wajibu wake wa kutafuta amani kwa kuendeleza mazungumzo, maridhiano, maelewano, kuheshimu utu na haki za kila mtu na watu na kwa matakwa ya sheria za kimataifa,” Papa alisititiza.

Mabalozi  wasio na makazi Vatican
Mabalozi wasio na makazi Vatican

Baba Mtakatifu aidha aliwaombia mabalozi hao kuwa:“ Kwa uwepo wake katika Jumuiya ya Kimataifa, Vatican, kwa mujibu wa asili na utume wake mahususi, unataka kuendeleza mazungumzo hayo katika huduma ya manufaa ya wote, bila kuendeleza malengo ya kisiasa, kibiashara au kijeshi. Kupitia "kutoegemea upande wowote", Vatican pia inajitahidi kuchangia utatuzi wa migogoro na masuala mengine kwa kuweka wazi mwelekeo wao wa asili wa maadili.” Papa alindelea kusema kwamba: “Historia imeonesha kwamba maendeleo mengi yanaweza kupatikana katika kutatua hali zinazoonekana kutoweza kusuluhishwa kwa njia ya utulivu, subira na juhudi za kidiplomasia zinazochochewa na kuheshimiana, nia njema na usadikisho wa maadili. Kwa hakika, matatizo mengi ya sasa ya kimataifa ni ya muda mrefu, ambayo badala ya kutuvunja moyo yanapaswa kutuchochea kutafuta masuluhisho mapya na ya kiubunifu.

Katika mtazamo mwingine Papa alisema “Katika siku hizi, mwaka huu  unapokaribia kuisha na tukingojea mapambazuko ya mwaka mpya, tunaalikwa kutazama wakati ujao kwa matumaini, tukiwa na “shauku na kutazamia mambo mema yajayo, licha ya kutojua wakati ujao unaweza kuwaje” (Rehje hati ya Jubilei  ya mwaka 2025, Spes Non Confundit, 1). Ni katika muktadha huo kwamba “ Tarehe 24 Desemba, nitazindua Mwaka wa Jubilei ya Kanisa wa 2025 kwa kufungua Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro.” Ujumbe mkuu wa Jubilei ni ule wa matumaini. Kanisa linapoanza hija ya tumaini lililofanywa upya kwa uwezo wa Kristo Mfufuka ili kufanya upya mambo yote (rej. Ufu 21:5), ninawatia moyo wanajumuiya ya wanadiplomasia walioidhinishwa na Vatican kuendelea kufanya kazi kwa ujasiri na ubunifu katika kukuza vifungo vya urafiki, ushirikiano na mazungumzo katika huduma ya amani.

Mabalozi wasio wakazi
Mabalozi wasio wakazi

Papa alikazia kusema kuwa "Kazi yenu mara nyingi tulivu na iliyofichwa, itasaidia kupanda mbegu za mustakabali wa matumaini kwa ulimwengu wetu uliochoshwa na vita." Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu  alisema mabalozi hao wapya wanapoanza kwa sasa utume wao mjini Vatican , anawatakia kila mmoja wao matashi mem ana sala huku akiwahakikisha kwamba Sekretarieti ya Vatican na Idara na Ofisi zingine za Curia Romana ziko tayari kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao. Na juu yao wote, wapendwa wao, na washiriki wa wafanyakazi wao, Papa amewapata Baraka nyingi za Mungu na kuwashukuru.

Mabozi wapya
07 December 2024, 11:37