Papa awatakia heri ya Noeli Curia Romana:tusihukumu wengine na vita huko Gaza ni ukatili!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mkutano wa Baba Mtakatifu Francisko na washiriki wa karibu wa Curia Romana, waliounganika pamoja katika kubadilishana matashi mema ya kiutamaduni ya Siku kuu za Noeli, tarehe 21 Desemba 2024, ulifunguliwa kwa kulaani ghasia mpya katika Ukanda wa Gaza, ambayo hata haiwaachi Watoto. Papa alianza kusema: “Kardinali Re alizungumza juu ya vita. Jana hawakumruhusu Patriaki kuingia Gaza (Hapa amezungumzia Patriaki Pierbattista Pizzaballa,)kama walivyoruhusu na na jana watoto walipigwa na mabomu. Huu ni ukatili. Hii sio vita. Ninataka kusema hili kwa sababu linagusa moyo. Asante kwa hilo. Asante.” Kichwa cha hotuba hii ni: “Wabariki, wala msilaani”(Hiki ni kifungu kutoka barua ya Rm 12,14 Papa alisisitiza mara mbili.
Shukrani zangu za dhati zimwendee Kardinali Re kwa salamu na matashi mema. Asante, kwa mfano wako wa utayari wa kutumikia na upendo wako kwa Kanisa. Curia Romana inaundwa na jumuiya nyingi zinazofanya kazi, ngumu zaidi au chini na nyingi. Mwaka huu, katika kufikiria tafakari inayoweza kunufaisha maisha ya kijumuiya katika Curia na ofisi zake mbalimbali, nilichagua kipengele kinacholingana vyema na fumbo la Umwilisho, na mtaona mara moja kwa nini. Nilifikiria kuwasema wengine vizuri na kutowasema vibaya. Hili ni jambo linalotuhusu sisi sote - maaskofu, mapadre, watu waliowekwa wakfu na walei. Katika suala hili, sisi sote ni sawa, kwa kuwa ni sehemu ya ubinadamu wetu.”
Kwa kuzungumza vizuri na kutosema vibaya ni onesho la unyenyekevu, na unyenyekevu ni alama ya Umwilisho na hasa fumbo la Kuzaliwa kwa Bwana ambalo tunakaribia kuadhimisha. Jumuiya ya kikanisa huishi kwa furaha na maelewano ya kidugu kiasi kwamba washiriki wake hutembea katika njia ya unyenyekevu, wakikataa kuwaza na kusemezana vibaya. Mtakatifu Paulo, akiandikia jumuiya ya Roma, alisema, “Barikini na wala msilaani”(Rm 12:14). Papa alisema kuwa “Tunaweza pia kuelewa maneno yake yanamaanisha nini: “Neneni vyema na msiseme vibaya” juu ya wengine, kwa upande wetu, wafanyakazi wenzetu, wakubwa wetu na wafanyakazi wenzetu, kila mtu.
Njai ta Unyenyekevu:kujishtaki
Katika kipengele cha “Njia ya unyenyekevu: kujishtaki, ”Papa Francisko kwa njia hiyo alipendekeza kuwa, kama alivyofanya miaka ishirini iliyopita kwenye Mkutano wa Jimbo huko Buenos Aires, kwamba “sisi sote, kama njia ya kuonesha unyenyekevu, tujifunze tabia ya kujilaumu, kama ilivyofundishwa na Walimu wa kiroho wa zamani, hasa Dorotheus wa Gaza. Ndiyo, Gaza, mahali pale pale panapolinganishwa na kifo na uharibifu, ni jiji la kale kabisa, ambako nyumba za watawa na watakatifu na walimu mashuhuri walisitawi katika karne za kwanza za Ukristo. Dorotheus alikuwa mmoja wao. Katika nyayo za Mababa wakuu kama Basil na Evagrius, alilijenga Kanisa kwa maandishi yake na barua zake, ambazo zimejaa hekima ya Kiinjili. Leo hii pia, kwa kutafakari mafundisho yake, tunaweza kujifunza unyenyekevu kupitia kujishtaki, ili tusiseme vibaya jirani zetu.”
Katika mojawapo ya “Maagizo” yake, Dorotheus alisema, “Uovu fulani unapompata mtu mnyenyekevu, mara moja anatazama ndani na kujihukumu kwamba amestahili. Wala hajiruhusu kuwashutumu au kuwalaumu wengine. Yeye huvumilia ugumu huu tu, bila kufanya fujo, bila uchungu, na kwa utulivu wote. Unyenyekevu haumsumbui yeye wala mtu mwingine yeyote” (Dorotheus wa Gaza, Mtazamo wa kiroho huko Paris 1963, kifungu 30). Na tena: “Usijaribu kujua makosa ya jirani yako au kuwa na tuhuma dhidi yake. Iwapo uovu wetu wenyewe unatokeza shuku hizo, jaribu kuzigeuza kuwa mawazo mazuri” (kifungu. 187). Kujishtaki ni njia tu, lakini ni muhimu. Ndio msingi wa kuweza kwetu kusema “hapana”’ kwa ubinafsi na “ndiyo” kwa roho ya kikanisa ya jumuiya. Wale wanaofanya tabia ya kujishutumu na kufanya hivyo mfululizo wanakombolewa hatua kwa hatua kutoka katika mashaka na kutoaminiana, na kutoa nafasi kwa Mungu, ambaye peke yake ndiye anayeweza kuunganisha mioyo. Ikiwa kila mtu atafanya maendeleo katika njia hiyo, jumuiya inaweza kuzaliwa na kukua, ambayo wote ni walinzi wa mtu mwingine na kutembea pamoja kwa unyenyekevu na upendo.
Ni nini msingi wa "mtindo" huu wa kiroho? Papa ameuliza na kujibu kwamba “Ni unyonge wa ndani, kwa kuiga (synkatábasis) au "kujishusha" kwa Neno la Mungu. Moyo mnyenyekevu unajinyenyekeza, kama moyo wa Yesu, ambaye katika siku hizi tunamfikiria kulala horini. Akiwa amekabiliwa na mkasa wa ulimwengu ulio katika mtego wa uovu, Mungu hufanya nini? Je! yeye huinuka katika haki yake yote na kutupa hukumu kutoka juu? Kwa maana fulani, ndivyo manabii walivyotarajia, hata wakati wa Yohane Mbatizaji. Lakini Mungu ni Mungu; mawazo yake si mawazo yetu, na njia zake si njia zetu (taz. Isa 55:8). Utakatifu wa Mungu, kama wa kimungu, ni wa kitendawili machoni petu. Aliye juu huchagua kujinyenyekeza, na kuwa mdogo, kama punje ya haradali, kama mbegu ya mtu ndani ya tumbo la mwanamke. Isiyoonekana.
Papa alisema kuwa “Kwa njia hiyo, anaanza kujitwika mzigo mkubwa na usiobebeka wa dhambi ya ulimwengu. Kujishusha kwa Mungu kunaakisiwa na mazoea yetu ya kujishtaki, ambayo kimsingi sio kitendo chetu cha maadili, lakini ukweli wa kitaalimungua, kama ilivyo kawaida katika maisha ya Kikristo. Ni zawadi kutoka kwa Mungu, kazi ya Roho Mtakatifu, ambayo ni juu yetu kukubali, "kujishusha" na kuwa tayari kukaribisha zawadi hii ndani ya mioyo yetu. Hivyo ndivyo Bikira Maria alivyofanya. Hakuwa na sababu ya kujishtaki, hata hivyo alichagua kwa hiari kushirikiana kikamilifu katika kujishusha kwa Mungu, katika kudhalilishwa kwa Mwana na kushuka kwa Roho Mtakatifu. Kwa maana hiyo, unyenyekevu unaweza kuitwa wema wa kitaalimungu.”
Tubarikiwe sisi wenyewe,tuwabariki wengine kwa zamu
Papa Francisko akiendelea na hotuba yake, alijikita na kipengele kingine cha “Tubarikiwe sisi wenyewe, tuwabariki wengine kwa zamu” na kusisitiza kuwa: “ Neno Kufanyika Mwili linatuonesha kwamba Mungu hajatuhukumu bali ametubariki. Zaidi ya hayo, anatufunulia kwamba ndani ya Mungu hakuna hukumu, bali ni baraka tu na daima. Hapa tunaweza kufikiria vifungu fulani vya Barua za Mtakatifu Catherine wa Siena, kama hii: "Inaonekana kwamba [Mungu] hataki kutokumbuka makosa yetu, au kutuhukumu kwa laana ya milele, lakini kutuonesha huruma ya kila wakati"(Barua, kifungu 15).“ Hata hivyo, juu ya yote tunaweza kufikiria juu ya Mtakatifu Paulo na maneno ya kwanza ya fahari ya wimbo unaopatikana mwanzoni mwa barua kwa Waefeso: “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye ametubariki kwa baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa roho katika Kristo”(Rej. Ef 1:3).
Hapa tunapata chimbuko la uwezo wetu wa "kuwabariki" wengine: hasa kwa sababu sisi wenyewe tumebarikiwa, tunaweza kubariki wengine kwa zamu. Sote tunapaswa kuzama katika undani wa fumbo hili; la sivyo tunahatarisha kukauka na kuwa kama mifereji iliyo tupu, iliyoboreshwa ambayo haina tena hata tone la maji. Kazi ya ofisini yenyewe mara nyingi ni kame na, kwa muda mrefu, inaweza kutufanya tukauke isipokuwa tukijiburudisha kupitia kazi ya uchungaji, nyakati za kukutana, urafiki, katika roho ya uwazi na ukarimu. Na hili liweze kutokea, tunahitaji, zaidi ya kitu kingine chochote, cha kufanya Mazoezi ya Kiroho kila mwaka katika kuzama katika neema ya Mungu, kuzamishwa kabisa na Roho Mtakatifu katika mafuriko yale ya maji ya uzima ambayo kila mmoja amepewa na kupendwa "tangu mwanzo."
Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa “Ikiwa mioyo yetu inakumbatiwa na baraka hiyo ya kwanza, basi tutaweza kubariki kila mtu, hata wale ambao hatuwajali au wale ambao wametutendea vibaya. Mfano ambao tunapaswa kutazama ni, kama kawaida, Bikira Maria, Mama yetu. Bikira Maria ndiye aliyebarikiwa. Hivi ndivyo Elizabeti anamsalimia katika ziara yake: "Umebarikiwa wewe kuliko wanawake, na mzao wa tumbo lako amebarikiwa!" ( Lk 1:42 ). Hivyo ndivyo sisi pia tunavyomwita katika “Salamu Maria.” Mama yetu alituletea “baraka ya kiroho katika Kristo” (rej. Ef 1:3) ambayo kwa hakika alikuwepo “mbinguni” kabla ya wakati wote, lakini pia, “katika utimilifu wa nyakati”, aliyokuwepo duniani, katika historia ya wanadamu. Neno likafanyika Mwili wa mwanadamu (taz. Gal 4:4). Kristo ndiye baraka hiyo. Yeye ndiye tunda linalobariki tumbo la uzazi; Mwana anayembariki Mama. Bikira Maria anaweza kushughulikiwa kwa usahihi, kwa maneno ya Dante, kama "binti wa Mwana wako." Maria, kama Mwenyeheri, alileta duniani Baraka ambayo ni Yesu.
Mafundi wa baraka
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake ndefu alijikita na kipengele cha kuwa 'mafundi wa Baraka’ kwamba “tunapomtazama Maria, sura na kielelezo cha Kanisa, tunaongozwa kutafakari juu ya mwelekeo wa kikanisa wa baraka hiyo. Hapo alipenda kufupisha kwa njia hii kwamba: katika Kanisa, ishara na chombo cha baraka za Mungu kwa wanadamu, sisi sote tumeitwa kuwa mafundi wa kubariki. Tunaweza kufikiria Kanisa kama mto mkubwa unaotiririka na kuwa vijito elfu moja na moja, vijito, vidogo kama bonde la Amazonia ambalo linanywesha dunia nzima kwa baraka za Mungu, zinazotiririka kutoka katika Fumbo la Pasaka ya Kristo. Kwa hiyo, Kanisa linaonekana kwetu kama utimilifu wa mpango ambao Mungu alimfunulia Ibrahimu tangu alipomwita mara ya kwanza kuondoka katika nchi ya babu zake. Bwana akamwambia, “Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, nami nitakubariki... na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa” (Mw 12:2-3). Mpango huo unatawala uchumi mzima wa agano la Mungu na watu wake, yaani watu "waliochaguliwa" sio kwa maana ya kipekee, lakini kwa maana ambayo sisi, kama Wakatoliki, tunaweza kuita "sakramenti."
Kwa neno moja, ni kutoa zawadi ya baraka hiyo kwa kila mtu kupitia mfano wetu, ushuhuda wetu, ukarimu wetu na uvumilivu wetu. Basi, katika fumbo la Umwilisho, Mungu amebariki kila mwanamume na mwanamke anayekuja katika ulimwengu huu, si kwa amri ya kunyesha mvua kutoka mbinguni, bali kupitia mwili wa Yesu, Mwana-Kondoo mbarikiwa aliyezaliwa na Maria mbarikiwa (rej. Mtakatifu. Anselm, 52). Baba Mtakatifu Francisko katika hilo alisema anavyotaka kufikiria Curia Romana “kama warsha kubwa ambayo kuna idadi yoyote ya kazi tofauti, lakini ambapo kila mtu anafanya kazi kwa madhumuni sawa ya: kubariki wengine, na kueneza baraka za Mungu na Mama Kanisa ulimwenguni. Hapa anadhani hasa kazi iliyofichwa inayofanywa na wafanyakazi wa ofisi hiyo the minutanti,kama wanavyoitwa hapo - ambao huandaa barua za kumhakikishia mtu ambaye ni mgonjwa au amefungwa, mama, baba au mtoto, mzee, na wengine wengi kwamba Papa anawaombea na kwamba anatuma baraka zake. Je, hiyo si kutumika kama fundi wa baraka?
Papa FRancisko alisema katika hilo kuwa "Waliniambia kwamba kuhani mtakatifu ambaye alifanya kazi miaka iliyopita katika Sekretarieti ya Vatican alikuwa amebandika nyuma ya mlango wa ofisi yake kipande cha karatasi kilichosomeka: "Kazi yangu ni ya unyenyekevu, na ya kufedhehesha." Pengine hii ilikuwa njia mbaya ya kuona mambo, ambayo si chembe ya ukweli na uhalisia wenye afya. Kwangu, inaweza kusomwa kwa njia chanya, kama vile kuwasilisha mtindo wa kawaida wa "mafundi" wa Curia Romana kuwa: unyenyekevu kama njia ya kueneza "baraka." Ni njia ya Mungu mwenyewe, ambaye katika Yesu anajishusha ili kushiriki katika hali yetu ya kibinadamu, na hivyo kutupatia baraka zake.” Papa Francisko alikazia kusema kuwa, “inatia moyo kufikiri kwamba kupitia kazi yetu ya kila siku, hasa ile iliyofichwa, kila mmoja wetu anaweza kusaidia kuleta baraka za Mungu ulimwenguni. Hata hivyo katika hili, ni lazima tuwe na msimamo: hatuwezi kuandika baraka na kisha kumsema vibaya kaka au dada yetu. Kwa hivyo nia yangu hii ni kwamba: Bwana, aliyezaliwa kwa ajili yetu kwa unyenyekevu, atusaidie daima kuwa wanaume na wanawake wa baraka. Ninawatakia Noeli Njema,” Papa alihitimisha hottuba yake.