Migogoro kila eneo, mlipuko huko Gaza. Papa anaomba kusitisha vita. Migogoro kila eneo, mlipuko huko Gaza. Papa anaomba kusitisha vita.  (ANSA)

Papa Francisko:wito wa kusitisha vita ili pande zote ziwe na amani katika Noeli

Baba Mtakatifu Fransisko,mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana,katika siku kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili tarehe 8 Desemba 2024 ametoa maombi kwa ajili ya nchi zilizoathirika na ghasia na kutoa wito wa kusitishwa ili amani duniani itawale hasa katika maadhimisho ya Noeli yanayokaribia.Ombi kwa ajili ya Nikaragua:Tutafute njia ya mazungumzo yenye heshima na yenye kujenga ili kukuza amani udugu na maelewano.Papa ameombea wafungwa Marekani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, tarehe 8 Desemba 2024, Baba Mtakatifu, mara baada ya misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican akiwa amezungukwa na  Makardinali wapya, waliovikwa kofia nyekundu tarehe 7 Desemba na kuwa sehemu ya Baraza la Makardinali rasimi, Makardinali, maaskofu wakuu, Maaskofu, Mapadre na waamini watu wa Mungu Papa alijongea katika Dirisha la Jumba la Kitume na kutoa tafakari yake kwa waamini ma mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Baada ya  Sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu alisema: Katika maadhimisho haya ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, niko karibu kwa namna fulani na Wanicaragua. Ninawaalika m muungane nami katika sala kwa ajili ya Kanisa na watu wa Nikaragua, wanaoadhimisha Mama wa Moyo Safi, kama Mama na Msimamizi  na kuinua kilio cha imani na matumaini kwake.  Mama wa mbinguni awe faraja kwao katika matatizo na mashaka, na kufungua nyoyo za wote, ili daima kutafutwa njia ya majadiliano yenye heshima na kujenga kwa ajili ya kuendeleza amani, udugu na maelewano nchini.”

Kuombea nchi zenye vita

Na tuendelee kuomba kwa ajili ya amani, katika Ukraine inayoteswa, katika Mashariki ya Kati - Palestina, Israel, Lebanon, sasa Syria -, katika Myanmar, Sudan na kila mahali panapokumbwa na vita na vurugu. Papa Francisko akiendelea ametoa wito “kwa Serikali na jumuiya ya kimataifa, ili tuweze kufikia sherehe ya Noeli kwa usitishaji wa mapigano kwa pande zote za vita.”

Salamu

Amewalimu Warumi  na mahujaji. Hasa, wanahija ya Wajumbe wa  Moyo Mtakatifu kutoka Hispania, kikundi cha "Oasi Mamma wa Upandeo,  waamini kutoka Marekani, Honduras na Australia; pamoja na wale kutoka Calderara ya Reno, Corpolò na Grado, na vijana  wa kipaimara kutoka parokia ya Mtakatifu  Pio wa Pietrelcina huko Roma.

Wafungwa Marekani na adhabu ya kifo

Papa Francisko mawazo yake moyoni yalikuwa ni kuwaomba wote kuwaombea wafungwa huko Marekani ambao wako kwenye korido ya kifo(yaani wanakabilia na adhabu ya kifo). Nadhani wako 13 au 15. Tuombe kwamba hukumu yao ya kifo  ibadilishwe. Hebu tuwafikirie hawa ndugu zetu na tumwombe Mungu awajalie neema ya kuwaokoa na kifo.”

Wakfu wa Chama cha Matendo ya Vijana Katoliki

Papa Francisko amewakumbuka walipyaisha wakfu wao  kwa chama cha Matendo ya vijana katoliki katika parokia za Italia. “Nawatakia wajumbe wote safari njema ya malezi, huduma na dhamana ya kitume."

Salamu nyingine

Ninawabariki kwa moyo wote waamini wa Rocca ya Papa na moto ambao watawasha  kama nyota hiyo kubwa kwenye Ngome ya mji wao mzuri, kwa heshima ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili. Papa Francisko alionesha ukaribu na wafanyakazi wa Siena, Fabriano na Ascoli Piceno ambao wanatetea kwa mshikamano haki ya kufanya kazi, ambayo ni haki ya utu! Kwamba kazi zao zisiondolewe kwa sababu za kiuchumi au kifedha. Papa amewatakia wote Dominika njema na sikukuu njema ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili. Na amewakaribisha tena alasiri katika Uwanja wa Hispania, mahali am,bapo Papa anatarajiwa kutoa heshima kwa kuweka dhada la Maua Chini ya Mnara wenye Sanamu ya Bikira maria. Na tafadhali msisahau kuniombea. Mlo mwema, mchana mwena na kwaheri ya kukuona!”

Baada ya Angelus
08 December 2024, 14:51