Papa Francisko,sala kwa Mama Maria:Utukoe na wivu maana sote ni ndugu!

Katika sala ya Papa kwa Mama Bikira Maria aliomba:"Mama yetu,Roma inajitayarisha kwa Jubilei mpya ambayo itakuwa ujumbe wa matumaini kwa wanadamu waliojaribiwa na migogoro na vita.Ndio maana kuna sehemu za ujenzi kila mahali katika jiji.Hii tunajua inasababisha usumbufu mwingi,lakini ni ishara kwamba Roma iko hai,inajipyaisha na kujaribu kukabiliana na mahitaji ili kukaribisha zaidi na kufanya kazi zaidi.Onyo:'kazi zisisonge roho ya Jubilei.'

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kama ilivyo utamaduni wa siku kuu ya Mkingiwa dhambi asili, katika jiji la Roma, Baba Mtakatifu Francisko tarehe 8 Desemba 2024 jioni alielekea katika Uwanja wa Hispania, mahali ambapo kuna mnara uliowekwa sanamu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili juu yake. Baada ya kufika hapo aliweka maua ambayo hata hivyo tangu alfajiri tayari chini ya mnara huo, waamini wengi na viongozi wa mamlaka ya Italia walikuwa wamekwisha toa heshima zao. Kwa njia hiyo Papa Francisko na waamini baada ya kuimba litania alisali sala kwa Mama Maria.

Papa Francisko katika uwanja wa Hispania
Papa Francisko katika uwanja wa Hispania

Bikira safi, Mama, Mama safi, leo ni sherehe yako na tunakusanyika karibu nawe.Maua tunayotoa tunataka kueleza upendo na shukrani zetu; lakini juu ya yote unaona na kuthamini maua hayo yaliyofichwa ambayo ni maombi, simanzi, hata machozi, hasa machozi ya wadogo na maskini. Watazame, Mama, waangalie. Mama yetu, Roma inajitayarisha kwa Jubilei mpya, ambayo itakuwa ujumbe wa matumaini kwa wanadamu waliojaribiwa na migogoro na vita. Ndio maana kuna sehemu za ujenzi kila mahali katika jiji: hii,  tunajua inasababisha usumbufu mwingi, lakini ni ishara kwamba Roma iko hai, kwamba Roma inajipyaisha, kwamba Roma inajaribu kukabiliana na mahitaji, ili kukaribisha zaidi na kufanya kazi zaidi.”

Meya wa Mji aliyeombewa na Papa yuko upande wake
Meya wa Mji aliyeombewa na Papa yuko upande wake

Lakini mtazamo wako wa Mama unaona zaidi. Na ninaona kama kusikia sauti yako ambayo inatuambia hivi kwa hekima: “Watoto wangu, kazi hizi ni sawa, lakini kuweni waangalifu: msisahau maeneo ya ujenzi wa roho! Jubilei ya kweli iko ndani: ndani, ndani ya mioyo yenu na unasema, ndani ya mahusiano ya familia na kijamii. Ni ndani ambayo tunahitaji kufanya kazi kujiandalia njia ya Bwana ajaye.”Na ni fursa nzuri ya kufanya maungamo mazuri na kuomba msamaha wa dhambi zote. Mungu husamehe kila kitu, Mungu husamehe daima. Mama safi, tunakushukuru! Pendekezo lako hili ni nzuri kwetu, tunaihitaji sana, kwa sababu, bila kutaka, tuna hatari ya kukamatwa kabisa katika maandalizi, katika mambo ya kufanya, na kisha neema ya Mwaka Mtakatifu wakati wa kuzaliwa upya kiroho, wakati wa msamaha na ukombozi wa kijamii, neema hii ya Jubilei inaweza isitoke vizuri, kwa kusongwa kidogo. Lakini hapa Meya anatayarisha mambo yote ili katika ukumbusho huu, katika Mwaka huu Mtakatifu, yawe mazuri. Tumuombee Meya ambaye ana kazi nyingi.

Hakika, Maria, utafikiri ulikuwapo katika sinagogi la Nazareti, siku ile Yesu kwa mara ya kwanza alipowahubiria watu wa nchi yake. Akisoma katika kitabu cha nabii Isaya: “Roho wa Bwana yu juu yangu; kwa sababu hii alinitia mafuta akanituma kuwahubiri maskini habari njema. kutangaza ukombozi kwa wafungwa na kuona kwa vipofu; kuwaweka huru walioonewa, kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” (Lk 4:18-19). Kisha akaketi na kusema: “Leo imetimia Maandiko haya mliyoyasikia” (Lk 4, 21). Na Wewe, Mama, ulikuwepo, kati ya watu walioshangaa. Ulijivunia Yeye, Mwanao, na wakati huo huo ulijizuia kufungwa na wivu, ambao huzalisha vurugu. Umepitia janga hili na kila mara ulilivuka, kwa moyo wako safi, kwa kujazwa na upendo wa Moyo wa Yesu. Mama, utuokoe kutoka katika wivu: kwamba sisi sote ni ndugu, na kwamba tupendane. Pasiwepo wivu. Wivu, uovu huo wa manjano, ambao ni mbaya, uharibifu kutoka ndani. Na hata leo, Mama, unarudia kusema nasi kuwa “Msikilizeni Yesu, msikilizeni Yeye! Msikilizeni na mfanye anachowaambia” (Yh 2:5). Asante, Mama Mtakatifu! Asante tena, wakati huu ni maskini wa matumaini, utupatie Yesu, Tumaini letu. Asante Mama. Papa Francisko alihitimisha.

Papa akiwa katika sala katika Uwanja wa Hispania
Papa akiwa katika sala katika Uwanja wa Hispania
Sala ya Papa mbele ya Sanamu ya Bikira Maria

 

08 December 2024, 16:45