Papa:huko Corsica nilifurahi kuona watu ambao wana watoto
Na Salvatore Cernuzio – Mwakilishi Ajaccio
Hakukuwa na mkutano na waandishi wa habari, kama kawaida katika kila Ziara yake ya 47 ya kitume, kwenye ndege ya kurudi kutoka Ajaccio hadi Roma. Sababu, muda ulikuwa mfupi mno wa kusafiri chini ya dakika 40. Na hii haijawahi kutokea katika safari nyingine za kimataifa za Papa, lakini pia haikuwahi kutokea kwamba safari hii ikawa fupi sana. Hata hivyo, mara tu alipoingia kwenye ndege, Dominika tarehe 15 Desemba 2024 hakutaka kukosa kuwasalimia waandishi wa habari 67 walioandamana naye katika masaa hayo kumi kwenye kisiwa cha Mediterania ili kushirikishana nao wazo pia. Au tuseme, maoni yake juu ya jambo ambalo lilimvutia zaidi kutoka katika ziara hiyo ya Ajaccio: idadi ya watoto walioonekana wakati wa mikutano mbalimbali, hasa kwenye Misa ya Uwanja wa Austerlitz, lakini pia mitaani mikononi mwao au karibu na wazazi wao.
Nchi inayozalisha watoto
Papa alianza kusema: "Nawashukuru sana kwa kazi zenu. Ningependa kusisitiza jambo moja: mmeona idadi ya watoto? Hii ni nchi inayotengeneza watoto, fikiria safari zingine ambazo humkuweza kuwaona. Katika Timor ya Mashariki na hapa - aliongeza Papa, akikumbuka moja ya hatua za safari yake ndefu ya mwezi Septemba Kusini-Mashariki mwa Asia na Oceania - nilifurahi kuona watu wanaozaa watoto. Huu ndio wakati ujao. Asante sana kwa kazi yenu," Papa alirudia kwa waandishi wa habari na wapiga picha. “Asante sana kwa hili. Tuonane safari ijayo!” "Wapi?" Waandishi wa habari waliuliza kutoka kwenye viti vyao. "Sijui!", Papa alijibu akitabasamu.
Safari hiyo fupi, hata hivyo, ilimwezesha Jorge Mario Bergoglio kupata wakati mdogo wa kusherehekea kwa zawadi ya keki kutoka kwa wanachama wa Aigav, chama cha wataalamu wa Vatican kilichoidhinishwa na vyombo vya habari vya kila bara ambao walitaka kusherehekea miaka 88 ya kuzaliwa kwa Papa mnamo Desemba 17.
Keki kutoka kwa waandishi wa habari wote
Keki hiyo, ya uwongo ("keki feki", mtu alitania), ilitengenezwa na maabara ya Kirumi ambayo iliitoa bure kwa kustaajabishwa sana na Papa wa Argentina: kwenye orofa tatu, ikiwa na rangi nyeupe na manjano ya bendera ya Vatican, ina maandishi "Hongera Papa Francisko", juu ya sanamu iliyo na papa aliyeketi na kidole gumba chake kilichoinuliwa, chini ya kadi "Heri na Siku ya Kuzaliwa yenye Furaha!"
Keki hiyo iliwasilishwa kwa Papa na mwandishi wa habari wa Mexico Valentina Alazraki doyen, mwandishi wa kihistoria wa Televisa Univision na rais mpya aliyechaguliwa wa Aigav, na safari 161 kwa Papa, katikati ya wimbo wa Happy Birthday" uliooimbwa na wenzake wa Ufaransa kumfuata Papa. "Waandishi wote wa habari wanakutakia heri ya siku yake ya kuzaliwa," Alazraki alisema wakati akikabidhi zawadi. "Ni bandia kwa hivyo kuwa na amani," aliongeza kwa mzaha, na vicheko vya waliohudhuria. Ikiwa ni pamoja na Papa ambaye alisema "asante" mara kadhaa, akiwabariki kwa mkono wake wale ambao katika miaka ya hivi karibuni amewafafanua kama "swasindikizaji wake wa kusafiri."