2024.12.15 Wakati wa kurudi kutoka Ajaccio 2024.12.15 Wakati wa kurudi kutoka Ajaccio  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:huko Corsica nilifurahi kuona watu ambao wana watoto

Kwa sababu ya muda kuwa mfupi mno wa safari ya ndege,Papa hakuwa na mkutano wa kawaida wa wanahabari waliosindikizana naye katika Ziara ya 47 ya Kitume huko Corsica.Hata hivyo,alitaka kushirikisha furaha yake ya kuona idadi kubwa ya wazazi wakiwa na watoto wao huko Ajaccio:“Ni nchi inayozaa watoto. Katika nchi nyingine hawakuonekana.Katika Timor Mashariki na hapa,ndiyo.Kwa Papa,keki ya kushtukiza kutoka kwa waandishi wa habari katika fursa ya siku yake ya kuzaliwa Desemba 17.

Na Salvatore Cernuzio – Mwakilishi Ajaccio

Hakukuwa na  mkutano na waandishi wa habari, kama kawaida katika kila Ziara yake ya 47 ya kitume, kwenye ndege ya kurudi kutoka Ajaccio hadi Roma. Sababu, muda ulikuwa mfupi mno wa kusafiri chini ya dakika 40. Na hii haijawahi kutokea katika safari nyingine za kimataifa za Papa, lakini pia haikuwahi kutokea kwamba safari hii ikawa fupi sana. Hata hivyo, mara tu alipoingia kwenye ndege, Dominika tarehe 15 Desemba 2024  hakutaka kukosa kuwasalimia waandishi wa habari 67 walioandamana naye katika masaa hayo kumi kwenye kisiwa cha Mediterania ili kushirikishana  nao wazo pia. Au tuseme, maoni yake  juu ya jambo ambalo lilimvutia zaidi kutoka katika ziara hiyo ya Ajaccio: idadi ya watoto walioonekana wakati wa mikutano mbalimbali, hasa kwenye Misa ya Uwanja wa Austerlitz, lakini pia mitaani mikononi mwao au karibu na wazazi wao.

Nchi inayozalisha watoto

Papa alianza kusema: "Nawashukuru sana kwa kazi zenu. Ningependa kusisitiza jambo moja: mmeona idadi ya watoto? Hii ni nchi inayotengeneza watoto, fikiria safari zingine ambazo humkuweza kuwaona. Katika Timor ya Mashariki na hapa - aliongeza Papa, akikumbuka moja ya hatua za safari yake ndefu ya mwezi  Septemba Kusini-Mashariki mwa Asia na Oceania - nilifurahi kuona watu wanaozaa watoto. Huu ndio wakati ujao. Asante sana kwa kazi yenu," Papa alirudia kwa waandishi wa habari na  wapiga picha. “Asante sana kwa hili. Tuonane safari ijayo!” "Wapi?" Waandishi wa habari waliuliza kutoka kwenye viti vyao. "Sijui!", Papa alijibu akitabasamu.

Papa akiwasalimia waandishi
Papa akiwasalimia waandishi

Safari hiyo fupi, hata hivyo, ilimwezesha Jorge Mario Bergoglio kupata wakati mdogo wa kusherehekea kwa zawadi ya keki kutoka kwa wanachama wa Aigav, chama cha wataalamu wa Vatican kilichoidhinishwa na vyombo vya habari vya kila bara ambao walitaka kusherehekea miaka 88 ya kuzaliwa kwa Papa mnamo Desemba 17.

Keki kutoka kwa waandishi wa habari wote

Keki hiyo, ya uwongo ("keki feki", mtu alitania), ilitengenezwa na maabara ya Kirumi ambayo iliitoa bure kwa kustaajabishwa sana na Papa wa Argentina: kwenye orofa tatu, ikiwa na rangi nyeupe na manjano ya bendera ya Vatican, ina maandishi "Hongera Papa Francisko", juu ya sanamu iliyo na papa aliyeketi na kidole gumba chake kilichoinuliwa, chini ya kadi "Heri na Siku ya Kuzaliwa yenye Furaha!"

AKIPOKEA keki
AKIPOKEA keki

Keki hiyo iliwasilishwa kwa Papa na mwandishi wa habari wa Mexico Valentina Alazraki doyen, mwandishi wa kihistoria wa Televisa Univision na rais mpya aliyechaguliwa wa Aigav, na safari 161 kwa Papa, katikati ya wimbo wa Happy Birthday" uliooimbwa na wenzake wa Ufaransa kumfuata Papa. "Waandishi wote wa habari wanakutakia heri ya siku yake ya kuzaliwa," Alazraki alisema wakati akikabidhi zawadi. "Ni bandia kwa hivyo kuwa na amani," aliongeza kwa mzaha, na vicheko vya waliohudhuria. Ikiwa ni pamoja na Papa ambaye alisema "asante" mara kadhaa, akiwabariki kwa mkono wake wale ambao katika miaka ya hivi karibuni amewafafanua kama "swasindikizaji wake wa kusafiri."

PAPA NA WAANDISHI
16 December 2024, 09:14