2024.12.11 Moja ya Picha ya Papa akiwa katika katekesi. 2024.12.11 Moja ya Picha ya Papa akiwa katika katekesi.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:Katika kitabu cha 'Spera' kuna kumbukumbu za maisha yake na wengine!

Katika siku yake ya kuzaliwa Papa akitimiza miaka 88,magazeti ya 'La Repubblica,Corriere della sera na The New York Times' yamechapisha baadhi ya muhtasari wa wasifu wa Papa unaoitwa‘ Spera.' Kitabu kitachapishwa tarehe 14 Januari 2025.Papa anazungumza juu ya utoto wake huko Buenos Aires.Anakumbuka ziara ya kihistoria ya Iraq mnamo 2021,huku kukiwa na shida za usalama na kuakisi uhusiano kati ya imani na ucheshi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mkusanyiko wa ubinadamu uliopatikana katika majengo ya kifahari ya Buenos Aires na jeraha la moyo lililowakilishwa na Iraq, aliyotembelea mnamo 2021, haya na zaidi yamo katika  wasifu wa  Papa Francisko unaoitwa "Spera", ulioandikwa na Carlo Musso,pamoja naye kitabu hicho, kitakachochapishwa tarehe 14  Januari 2025 katika zaidi ya nchi mia moja ulimwenguni. Tarehe 17 Desemba 2024, siku ambayo Papa ametimiza miaka 88, magazeti ya Italia ‘La Repubblica’, ’Il Corriere della Sera’ na New York Times  yamechapisha baadhi ya dondoo za kitabu hicho.

Utoto katika kitongoji cha Flores

Baba Mtakatifu Francisko, akikumbuka katika kumbukumbu yake kwamba mchanganyiko, wa makabila mengi, wa kidini na wa tamaduni nyingi unaowakilishwa na Flores barrio, kitongoji cha Buenos Aires ambapo utoto wake ulianzia kwamba “mtu anaponiambia kuwa mimi ni Papa wa Villero, ninaomba tu kwamba ninastahili. Hapo tofauti zilikuwa za kawaida na tuliheshimiana," anakumbuka Bergoglio, akikumbuka vikundi vya marafiki Wakatoliki, Wayahudi na Waislamu, bila tofauti.

"Magdalenes wa kisasa"

Papa anakumbuka kukutana kwake na makahaba, taswira ya upande wa giza na wa kuchosha zaidi ambao ameujua tangu alipokuwa mtoto katika vitongoji vya Argentina. Baada ya kuwa Askofu, Bergoglio aliadhimisha Misa kwa baadhi ya wanawake hao ambao walikuwa wamebadilisha maisha yao wakati huo huo. “Nimekuwa kahaba kila mahali, mmoja wao, anayeitwa Porota, hata nchini Marekani. Nilipata pesa, kisha nikapendana na mwanaume mzee, alikuwa mpenzi wangu, na alipokufa nilibadilisha maisha yangu. Nina pensheni sasa. Na ninakwenda kuwaogesha wazee na vikongwe kwenye nyumba za wazee wasio na mtu wa kuwatunza. Siendi sana kwenye Misa, na nimefanya kila kitu kwa mwili wangu, lakini sasa ninataka kutunza miili ambayo hakuna mtu anayeijali,” alimwambia mmoja wa makahaba.  Katika hilo, Papa Francisko anamfafanua kuwa “Ni Magdalena wa kisasa." Porota atamwita kwa mara ya mwisho, kutoka hospitalini, muda mfupi kabla ya kufa, ili kupokea Upako wa Wagonjwa na Komunio. Papa anaandika “Ilienda vizuri kama watoza ushuru na makahaba ambao wanatutangulia katika ufalme wa Mungu" (Mt 21,31). Na nilimpenda sana. Hata sasa, siku ya kifo chake, sisahau kumwombea.”

Urafiki na baba Pepe

Kuna  kumbukumbu nyingi  za wafungwa, ambao walitengeneza brashi kwa nguo, na pia historia ya kuzaliwa kwa urafiki na Padre  José de Paola, anayejulikana kama ‘Baba Pepe’, kuhani wa Parokia ya Virgen de Caacupé, (Bikira) huko Villa 21, na kuungwa mkono na usikilizaji na ukaribu kutoka kwa Papa wa siku zijazo katika wakati wa shida ya kitaaluma. Katika maeneo yale yaliyo pembezoni mwa jiji, ambako Serikali imekosekana kwa miaka arobaini na ambapo utumiaji wa  dawa za kulevya ni janga linalozidisha hali ya kukata tamaa, papo hapo, Papa alisisitiza tena katika vitongoji hivyo ambavyo lazima vizidi kuwa kitovu kipya cha Kanisa, kundi la walei na mapadre kama Padre Pepe wanaishi na kutoa ushuhuda wa Injili kila siku, kati ya watu waliotupiliwa mbali na uchumi unaoua. Ukweli mgumu ambao unajitokeza wazi kwamba dini sio  kama wengine wanavyosema,  kuwa kasumba ya watu, historia ya  kutia moyo ya kuwatenganisha watu. Hakika: ni shukrani kwa imani na kujitolea kwa uchungaji na kiraia kwamba majengo ya kifahari yameendelea kwa njia isiyofikirika, licha ya matatizo makubwa. Na kama vile imani, kila huduma ni mkutano kila wakati, na ni sisi juu ya wote ambao tunaweza kujifunza mengi kutoka kwa maskini.

Ziara ya Iraq na jeraha la moyo la Mosul

Kuanzia majanga ya kutisha katika  vitongoji vya mijini hadi majanga ya Iraq iliyoharibiwa na migogoro, mtazamo wa Papa Francisko haubadiliki, lakini daima unabakia kuwa uwaangalifu na kuwajali wanadamu waliojeruhiwa. Katika ziara hiyo ya kihistoria iliyofanywa kuanzia tarehe 5 hadi 8 Machi 2021 ya kwanza ya Papa nchini  humo alikumbuka jeraha la moyo lililowakilishwa na Mosul: Moja ya miji kongwe zaidi ulimwenguni, iliyojaa historia na mila, ambayo imeona urithi wa ustaarabu tofauti kwa wakati na ilikuwa ishara ya kuishi kwa amani kwa tamaduni tofauti katika nchi moja. Waarabu, Wakurdi, Waarmenia, Waturukimeni, Wakristo, Wasiria, walijidhihirisha machoni pangu kama eneo la vifusi, baada ya miaka mitatu ya kukaliwa na Dola ya Kiislamu, ambayo ilikuwa imeichagua kuwa ngome yake. Na wakati wa kuruka kutoka juu na helikopta, eneo hilo lilionekana kama ‘x-ray’ ya chuki, mojawapo ya hisia za ufanisi zaidi za wakati wetu.

Katika safari hiyo, Papa Francisko alikumbuka muktadha mgumu wamaandalizi, kwa sababu ya kuendelea kwa Janga la Uviko -19 na suala la usalama. “Nilikuwa nimeshauriwa dhidi yake na karibu kila mtu... lakini nilihisi kwamba nilipaswa kwenda kwenye nchi ya Ibrahimu, wasindikizaji  pamoja ya Wayahudi, Wakristo na Waislamu.” Bergoglio hakuficha taarifa iliyopokelewa kutoka idara za siri za Kiingereza kuhusu mashambulizi mawili yaliyotayarishwa wakati wa ziara yake mjini Mosul. Mmoja wa washambuliaji alikuwa mwanamke, aliyejaa mabomu na mwingine alikuwa ndani ya gari. Wote wawili walikuwa wamenaswa na kuuawa na polisi wa Iraq kabla ya kufanikiwa katika lengo lao. Hili pia lilinigusa sana. Hili pia lilikuwa tunda lenye sumu la vita.

Ushauri wa kutanguliza akili, na sio migogoro

Katika chuki hiyo yote, hata hivyo, Papa aliona nuru ya matumaini katika mkutano na Ayatollah Ali al-Sistani, tarehe 6 Machi 2021 huko Najaf, katika  mkutano ambao anabainisha kywa ulikuwa umetayarishwa kwa miongo kadhaa,  ambao ulifanyika katika mazingira ya kidugu pale pale nyumbani kwa al-Sistani na " Ishara ambayo Mashariki ni fasaha zaidi kuliko matamko au hati, kwani inamaanisha urafiki, wa familia moja. Ilikuwa nzuri kwa roho yangu na ilinifanya nijisikie kuheshimiwa," anandika Papa. Kuhusu Ayatollah, Papa anakumbuka hasa himizo la pamoja kwa mataifa makubwa ya kuachana na lugha ya vita, na kutoa kipaumbele kwa akili na hekima. Na kisha maneno, aliyabeba pamoja kama zawadi ya thamani kwamba: "Binadamu ni ndugu kwa dini au sawa kwa uumbaji.” Mbali na kitabu cha Spera, maisha ya Papa Francisko pia yatasimuliwa katika filamu inayohusu Maisha. Historia yangu katika Historia, wasifu ulioandikwa  na Fabio Marchese Ragona na kuchapishwa Machi mwaka 2023 na Nyumba ya uchapishaji ya HaperCollins.

Ucheshi ni dawa dhidi ya kujifunga binafsi

Gazeti la New York Times pia lilichapisha dondoo kutoka kwenye wasifu ambao  Papa Francisko anazungumzia kuhusu uhusiano kati ya imani na ucheshi. Maisha bila shaka yana huzuni yake, ambayo ni sehemu ya kila safari ya matumaini na kila safari kuelekea uongofu. Lakini ni muhimu kuepuka kugaagaa katika hali ya huzuni kwa gharama yoyote ile, na kutoiruhusu kuumiza moyo, alisema Papa, ambaye anakumbuka kwamba ingawa baadhi ya makasisi katika Kanisa ni wenye kiburi kuliko furaha, hata hivyo tunaelekea kuwa na hisi ucheshi na hata mkusanyiko mzuri wa vicheshi na hadithi za kuchekesha. Na hapa Papa Fransisko anataja baadhi ya historia kuhusu Yohane XXIII na Yohane Paul II  ambaye  mwishowe  alikaripiwa na Kardinali mmoja wakati wa vikao vya awali vya Mkutano Mkuu kwa ajili ya kupanda milima, kuogelea na kuendesha baiskeli (Kwa upande wake alikuwa amesema: "Siamini kwamba hizi ni shughuli zinazofaa kwa jukumu lako", na wakati huo huo, Papa Yohane Paulo II alikuwa amemjibu kwa ucheshi tu kwamba: "Lakini unajua kuwa huko Poland hizi ni shughuli zinazofanywa na angalau asilimia 50% ya Makardinali? .... cha hajabu ni kwamba "huko Poland, wakati huo, kulikuwa na makardinali wawili tu...". Papa Francisko akiwa na maana ya matani aliongeza: "Kejeli ni dawa ambayo husaidia kushinda jaribu la ujinga," haya yamo katika kifungu cha maandishi kilichochapishwa katika Gazeti la New York Times.

Katika maandishi mengi yanaishia na historia  kidogo juu ya Papa Francisko mwenyewe ambaye, baada ya kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa New York wakati wa Ziara yake ya Kitume alimweleza dereva aliyekuwa akimsubiri kwamba je ninaweza kupanda mwenyewe na kaa nyuma ya gari hilo. Na wakati, akizidisha mwendo kasi, dreva alisimamishwa kando ya barabara na Polisi aliyemuuliza hati zake wakati akipiga hatua zake, huku kule akichungulia na upekuaji wake na kuuliza taarifa juu ya ndani ya gari kwamba lazima kuna mtu ambaye ni muhimu sana. Na kwa kuwa Polisi hakujumuisha kwamba inawezekana kuwa ni meya, gavana au rais, kwa swali lake dreva alisema: "Na ni nani anayeweza kuwa muhimu zaidi kuliko rais?" Dreva alijibu: "Tazama, bosi, sijui yeye ni nani hasa, bali ninachoweza kukuambia  tu ni kwamba ni Papa ninayemwendesha!"...

Ndondoo za Kitabu cha Papa "Spera"
17 December 2024, 18:35