Papa:Injili iwafikie wote na kuepuka maneno!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na watawa wakarmeli wajumbe wa Roho Mtakatifu tarehe 6 Desemba 2024 mjini Vatican. Alifurahi kukutana nao na wametoka mbali huko Brazil, lakini hata sehemu mbali mbali za Ulaya. Uwepo wao alisema ina maana kubwa zaidi katika wakati huu, wa mkesha wa Mwaka wa Jubileo. Baba Mtakatifu Francisko alisema kwamba katia maana hiyo kamili inayofanana na Injilishaji ambayo inaonisha Yesu katika Sinagogi ya Nazareth na ambayo imeuhishwa na Mwanzo wa Shirika lao: Roho wa Bwana yu juu yangu (…) na amenituma(…) kutangaza mwaka wa Neema(Lk 4,18…). Lakini hata mwaka huu ambao unakaribia kuisha tayari kweli ni mwaka wa neema kwao kwa sababu mwezi Julai waliadhimisha miaka 40 ya kuanzishwa kwa shirika lao,sanjari na Mkutano wao Mkuu IV. Ambapo walichagua kikundi cha kuongoza familia yao ya kitawa kwa miaka sita.
Katika fura hiyo nzuri, Baba Mtakatifu aliwaeleza kuwa ni vizuri kukumbuka jitihada za kila siku katika huduma ya Uinjilishaji na kueneza Neno la Mungu ambalo lazima liwafikiwe wote. Kiukweli kutangaza Injili duniani kote ni utume kwa wakristo wote. Papa Francisko aliongeza kusema: Ni maneno ya Mtakatifu Paulo ambayo anapaswa kukung’uta katika mioyo ya kila mbatizwa yasemayo: “ole wangu nisipotangaza Injili (1Kor 9,16).
Katika hilo Papa ametoa mfano kwamba," tunaona watawa wa kike na kiiume ambao badala ya kutangaza Injili wanafanya maneno ya kuendelea. Lakini ninyi msifanye hivyo. Kwa sababu maongezi ni kinyume cha kutangaza Injili, kwa sababu maongezi daima ni laana ya mwingine, kwa kumsengenya yule. Badala yake Injili inakaribishwa kila mara: ikisema: “Njoo, njoo.” Iwapo wakati fulani itatokea kwamba baadhi yenu wataingia kwenye gumzo hili, tafadhali msaidie atoke humo haraka iwezekanavyo,” Papa ameshauri. Kwa njia hiyo Papa alendelea alisema kuwa katika Taasisi yao ari hiyo ya kimisionari ya uinjilishaji katika mantiki hiyo ni kuunganishwa moja kwa moja na kufakari na kwa maisha ya sala ya kina ambayo inafuata ukale na tamaduni nzuri ya kikarmeli. Amewaapa Baraza na kwamba Mama yetu wa Aparecida awalinde.