Papa kwa Manos Unidas:Maria ndiye kielelezo cha utume!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko akikutana mjini Vatican, Jumatatu tarehe 9 Desemba 2024 aliwasalimu washiriki wa kikundi cha Manos Unidas yaani (kuunganisha mikono) kwenye kumbukumbu ya miaka 65 ya kuanzishwa kwa kikundi, ambapo pia Papa alitambua unyeti na ujasiri unaofaa kwa fikra ya kike ambao unaashiria kazi yao ya kukuza maendeleo katika nchi zinazoendelea. Baba Mtakatifu katika hotuba yake alibainisha kuwa Manos Unidas (Kampeni ya Kikatoliki dhidi ya Njaa Ulimwenguni)iliibuka kama jibu la Wanawake wa Chama cha Matendo ya Kikatoliki nchini Hispania kwa ombi la FAO mnamo 1959 ili kutoa mkate katika njaa ya utamaduni, kwa watu wa Mungu ambao sehemu kubwa ya wanadamu inateseka.
Katika tafakari yake juu ya kazi ya Manos Unidas, na usikivu na ujasiri unaofaa kwa fikra ya kike ambayo wanaifanya, mawazo ya Papa yalielekezwa kwa Bikira Maria kwa sababu, alisema, “Bikira Maria ni Mwanamke bora. Maria ndiye kielelezo kikamilifu cha ubinadamu wetu, ambaye kupitia kwake, kwa neema ya Mungu, sisi sote tunaweza kuchangia kuboresha ulimwengu.” Papa Francisko aidha alisisitiza kwamba hili ni lengo la Manos Unidas, lililofanywa kwa tabia angavu na ukweli" ya akina mama, mabinti na wanawake ambao wanaunda kundi hilo.
Dhamira mahususi ya shirika la kupambana na njaa, maendeleo duni na ukosefu wa elimu, iliyofanywa kwa huruma na ushupavu unaoonesha roho ya kike inawezekana kuwa maono ya Kikristo ya mwanadamu. Kwa hiyo Papa Francisko alititiza kuwa kwa kuwahimiza wanachama wa Manos Unidas kuendelea na kazi yao hasa ujumbe mzuri wa huduma na usaidizi wa hiari, huku akiwaalika kushiriki katika mwaka ujao wa Jubilei kama "mahujaji wa matumaini" na mchango wao katika uboreshaji wa nyenzo, maendeleo ya maadili, na maendeleo ya kiroho ya wale walio dhaifu na wahitaji. Hatimaye, Baba Mtakatifu aliwatakia matashi mema katika kipindi cha majilio kwa matumaini kwamba kipindi hikicha kutarajio ahadi za Mungu, kinaweza kutusaidia sote kufikia upya wa kiroho ili kuchangia katika ujenzi unaotamaniwa wa ustaarabu wa upendo.