2024.12.16 Wawakilishi wa Viongozi na wafanyakazi katika Taasisi za Benki za mikopo nchini Italia. 2024.12.16 Wawakilishi wa Viongozi na wafanyakazi katika Taasisi za Benki za mikopo nchini Italia.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa taasisi za Benki Italia:Ni lazima kukuza uchumi wa amani

Akikutana na wajumbe kutoka kwa baadhi ya taasisi za benki za Italia Papa alisisitiza kwamba wakati kigezo katika benki kinakuwa faida,kuna matokeo mabaya katika uchumi na amekosoa mashirika ya kimataifa yanayohamisha shughuli hadi mahali rahisi pa kunyonya na kuziweka familia na jamii katika shida.Taasisi za benki zina majukumu makubwa ya kuhimiza mantiki jumuishi na kusaidia uchumi wa amani.Jubilei inayokaribia inatukumbusha hitaji la kusamehe madeni.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 16 Desemba 2024 akikutana mjini Vatican na Marais, Bodi za Wakurugenzi na wawakilishi wa taasisi  za benki  za mikopo nchini Italia amewakaribisha na kwamba  mkutano huu umempatia  fursa ya kutafakari juu ya uwezo na kinzani za uchumi wa sasa na fedha. “Kanisa limeonesha umakini wa kipekee kwa uzoefu wa benki katika ngazi maarufu, na mara nyingi wanaume na wanawake wanaohusika katika jumuiya ya kikanisa wamekuza na kuunda Monti di pieta, benki, taasisi za mikopo za ushirika na benki za vijijini.” Lengo daima limekuwa kutoa fursa kwa wale ambao vinginevyo wasingeweza kuwa na hali nzuri na hivyo hilo ni jambo zuri la kufungua mlango wa fursa. Ni nzuri sana!

Katika nusu ya kwanza ya karne ya 15, na kuzaliwa kwa ‘Monti di Pieta,’ Ufransiskani  ulikuwa umetoa umuhimu wa wazo la uwepo wa watu maskini katika jiji kuwa ni ishara ya ugonjwa wa kijamii. Na hii ni kweli hata leo. Benki ya Monti di pieta na Monti frumentari zilitoa mikopo kwa wale ambao hawakuweza kumudu na kuruhusu familia nyingi kurudi kujisimamia  na kuunganishwa katika shughuli za kiuchumi na kijamii za jiji. Kati ya karne ya kumi na tisa na ishirini, pia kufuatia na kuchapishwa kwa Waraka wa Rerum Novarum ya Papa  Leo XIII, kitu kama hicho kilipatikana katika nchi ya Italia. Uchumi unaohusishwa na eneo hilo umeendelea kutokana na mpango wa mapadre walioelimika na walei.

Mikopo ya Benki inaweza kusaidia shughuli za uchumi

Mikopo ya benki imeweza kusaidia shughuli nyingi za kiuchumi, katika nyanja za kilimo na ile ya viwanda na biashara. Baba  Mtakatifu amesema kuwa “Kumbukumbu ya matukio haya hutumika kuelewa utata unaoathiri njia fulani ya kufanya benki na fedha katika wakati wetu. Kwa bahati mbaya, katika ulimwengu wa utandawazi, fedha hazina sura tena na zimejiweka mbali na maisha ya watu. Wakati kigezo pekee  kinakuwa ni faida, tuna matokeo  yake yanakuwa mabaya kwa uchumi halisi. Kuna mashirika ya kimataifa ambayo yanahamisha shughuli hadi mahali ambapo ni rahisi kutumia nguvu kazi, kwa mfano, kuweka familia na jamii katika matatizo na kufuta ujuzi wa kazi ambao umejengwa kwa miongo kadhaa.

Papa aidha alisema kuwa “Na kuna aina ya fedha ambayo inahatarisha kutumia vigezo vya riba, inapopendelea wale ambao tayari wamehakikishiwa na kuwatenga wale walio katika shida na wangehitaji kuungwa mkono na mkopo.” Na hatimaye, kuna hatari tunayoona ambayo ni umbali kutoka katika maeneo. Kuna fedha inayokusanywa  kutoka sehemu moja na kuhamishia rasilimali hizo katika maeneo mengine kwa lengo moja tu la kuongeza maslahi yake. Kwa hiyo watu wanahisi kuachwa na kunyonywa.” Wakati fedha inapokanyaga watu, inachochea ukosefu wa usawa na kujitenga na maisha ya ndani, inasaliti kusudi lake. Papa ameongeza “ningesema, inakuwa, uchumi usio na ustaarabu.”

Kuna kiharusi cha uchumi

Kwa hiyo uwepo wao naye  Papa Francisko amebainisha kuwa “unazungumza juu ya utofauti katika ulimwengu wa uchumi na benki.” Wao wana historia na miundo tofauti ya kukidhi mahitaji ya watu mbalimbali. Kiukweli, bila mifumo ya kutosha ya kifedha, yenye uwezo wa kujumuisha na kukuza uendelevu, hakutakuwa na maendeleo fungamani ya binadamu. Uwekezaji na usaidizi wa kazi haungewezekana bila jukumu la upatanisho la kawaida la benki na mikopo, kwa uwazi unaohitajika.” Kila wakati uchumi na fedha una athari thabiti kwenye maeneo, kwa jumuiya ya kiraia na kidini, kwa familia, ni baraka kwa kila mtu. Fedha ni kidogo kama "mfumo wa mzunguko", kwa kusema, wa uchumi: ikiwa unazuia katika baadhi ya vipengele na hakuna kuenea katika kiungo kizima cha kijamii, mashambulizi ya moyo na kiarusi cha uchumi wenyewe hutokea. Ufadhili wa afya haupunguzi katika mitazamo ya ulafi, uvumi safi na uwekezaji unaoharibu mazingira na kuhimiza vita.

'Uzito wa siku lazima usambazwe sawa katika mabega'

Papa Francisko alisema kuwa taasisi za benki zina majukumu makubwa ya kuhimiza mantiki jumuishi na kusaidia uchumi wa amani. Jubilei iliyo juu yetu inatukumbusha hitaji la kusamehe madeni. Ni hali ya kuzalisha matumaini na mustakabali katika maisha ya watu wengi hasa maskini. Papa amehimiza kupanda ujasiri. Kwa njia hiyo wasichoke kuandamana na kuweka kiwango cha haki ya kijamii juu. Hivi ndivyo Padre Primo Mazzolari aliandika: "Uzito wa siku lazima usambazwe kwa usawa katika mabega yote wanayoweza kubeba. Uadilifu huu wa awali unapatikana kwa kuelimisha dhamiri - kuelimisha dhamiri! - kwa hisia ya kina na nyeti ya uwajibikaji wa kijamii, ili kukwepa mchango wa wajibu wa kazi na juhudi kwa manufaa ya wote kunachukuliwa kuwa ni aibu na kuhukumiwa na maoni ya umma kama ukosefu wa uaminifu." Papa amewatakia wabebe matumaini ya wengi wanaowageukia wakijaribu kuamka kutoka kwenye vipindi vigumu au kuzindua upya shughuli zao za ujasiriamali. Amewabariki wote  na familia zao  za ,wapendwa wao.

16 December 2024, 16:24