2024.12.20 Watoto wa Chama cha Matendo ya kikatoliki cha vijana Italia (ACR). 2024.12.20 Watoto wa Chama cha Matendo ya kikatoliki cha vijana Italia (ACR).  (Vatican Media)

Papa kwa vijana:Noeli ni Siku Kuu lakini katika chakula tukumbuke wanaoteseka!

Papa Fransisko akikutana na Jumuiya ya Chama cha Matendo ya Vijana Kikatoliki aliwahimiza wajionee kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu kama"habari njema" ambayo kila mwaka hupyaisha roho na moyo".Amewaomba wasipoteze uwezo wa kushangaa na kuwa na mshikamano na vijana wengi ambao wanakabiliwa na njaa,vita, magonjwa,hasa wale wa Ukraine.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko  amekutana na vijana wa Chama cha Matendo ya vijana Wakatoliki wa Italia(ACR), katika fursa ya kutakiana heri ya Noeli, Ijumaa tarehe 20 Desemba 2024. Amewashukuru kufika kwao tena mwaka huu kwa salamu za Noeli! Amewasalimu Rais wa Taifa na Msaidizi Mkuu, viongozi, waelimishaji, anawasalimu wote. Wamechagua mada: "Kuingia ndani kabisa" kama mwongozo wa safari ya mafunzo ya mwaka huu. Hili mara moja linawakumbusha wanafunzi wa kwanza wa Yesu, waliokuwa wavuvi; na Yesu akawafanya kuwa “wavuvi wa watu”(rej. Lk 5:1-11). Kwa hiyo alipenda kutafakari na wao kwa muda juu ya picha hizi mbili za ‘uvuvi’ na ‘mshangao.’ Papa amesisitiza jambo la kwanza la kuwa wavuvi wa watu. Je ina maana gani? Labda kukamata watu, labda kwa kutumia mitandao ya kisasa zaidi? Hakika hii sivyo Bwana anataka. Mungu hataki “kumteka” mtu yeyote, kwa sababu anaheshimu uhuru wetu. Badala yake anatoa upendo wake na wokovu kwa kila mtu, bila kutarajia malipo yoyote na bila kutengwa.

Vijana wa ACR
Vijana wa ACR

 

Anashiriki nasi furaha yake ya kuwa Mwana mpendwa wa Baba: “Yesu anatuambia.  Nina Baba wa ajabu, ambaye anapenda kila mtu, bila mipaka, na ninataka kumjulisha na wewe pia, ili uwe na furaha pamoja nami!” Hivi ndivyo Yesu anatenda kama “mvuvi wa watu”: akiwaambukiza kwa furaha na ajabu ya upendo wake. Na hii inatuleta kwenye hatua ya pili: mshangao, kujua jinsi ya kushangaa.  Papa amewauliza kama huwa wanaona watu wanaoka? Kuna wengine... Na wanajua ni kwa nini? Kwa sababu watu hawa hawajui kushangaa! Kila kitu kiko hivi, kila kitu ni sawa, hawa wanapoteza uwezo wa kushangaa.” Papa alisema kuwa “Noeli ni wakati wa pekee kwa maana hiyo: mitaa imejaa taa, zawadi zinabadilishwa, liturujia hutajiriwa na nyimbo na sauti nzuri. Watoto na vijana wa Chama cha matendo Katoliki ambao walifika hata kuimba. Kila kitu ni kizuri, sivyo? Hebu tufikirie kuhusu Pango  la Kuzaliwa kwa Yesu: kuna mshangao kiasi gani. Papa aliwauliza kwa kufikiria: “Wachungaji, Mamajusi na wahusika wengine wanazunguka pango kwa nyuso zao za mshangao, wakihusisha hata wanyama na mazingira yote kana kwamba ni katika sherehe kubwa. 

Papa amewapa ushauri wa kusimama mbele ya Pango la kuzaliwa na walitazame kwa makini; kisha waende kutazama jingine kwa makini... Kuna aina mbalimbali katika zote, Mapango ya kuzaliwa kwa Bwana ya Napoli ni mazuri! Lakini katika yote hayo Yesu, Maria na Yosefu bila kukosa: upendo huo ambao Mungu alitutumia sisi na Maria na Yosefu ambao wanamtunza. Papa amewaomba wawe waangalifu kwa sababu hiyo haitumiki kwa Noeli tu. Bali katika maisha yetu yote, kiukweli, ni zawadi isiyo ya kawaida: kila mmoja wetu ni wa kipekee na kila siku ni wa kipekee, kama Mwenyeheri Carlo Acutis alivyopenda kusema. Papa Francisko amewauliza kama wanamjua, na walimjibu ndiyo. Yeye alipenda kusema kuwa: “lazima tuwe asili na siyo nakala.” Na ni watu wangapi ambao hawana uwezo wa kuwa wa asili, bali ni nakala! Kwa kuongezea: “Leo hii inafanywa kwa sababu gazeti linasema ni lazima ifanywe au kutoka katika mazoea.” Na Noeli ni nakala ya vitu vingi, kwa watu wengi na sio mkutano -mzuri sana! ambao kila mwaka hutuletea mambo mapya, kwa nafsi na moyo wa kila mmoja wetu.”

Papa na ACR
Papa na ACR

Kwa kutazama Pango la kuzaliwa kwa Yesu, kutazama Maria, Yosefu na Mtoto, Mamajusi, wachungaji, watu wanyenyekevu, wanaokwenda kumwangalia Yesu. Hebu basi tujifunze kushangaa. Tafadhali tusipoteze uwezo wa kushangaa. Tujifunze kutochukua kitu chochote kuwa cha kawaida, hasa upendo: ule wa Mungu na wa watu tunaokutana nao. Tunaambukiza kila kitu na kila mtu kwa maajabu yetu: kutoka nyumba hadi nyumba ya jirani, kutoka parokia hadi parokia nyingine, kutoka jiji hadi jiji jingine, kutoka taifa hadi taifa lingine. Hivi ndivyo tunavyoeneza furaha, uaminifu na faraja. Noeli ni habari njema. Sio kuwa na chakula cha jioni kikubwa au chochote zaidi. Tunaweza kuwa na chakula cha jioni kikubwa, ni kizuri; na  familia, lakini pia mambo mengine: tukitazama Pango la kuzaliwa, tunakwenda kanisani. Ni siku kuu ambayo ni mzizi wa imani yetu,” Papa alihimiza.

Papa Francisko aliwaeleza anavyojua jinsi ambavyo wameleta zawadi kwa ajili ya wale wanaohitaji zaidi. Kwa njia hiyo alongeza: “Msiwasahau masikini na mnapowakuta watoto wenye shida, watu masikini, watazameni machoni na muwaguse mikono yao mnapotoa sadaka; kuwa karibu sana, kwa  ukaribu huo tu ambao upendo hutoa. Na Maria na Yesu walikuwa wahitaji.”  Papa Francisko ameuliza tena swali: “Je ni yupi kati yenu anayekwenda kujifungulia katika sehemu ambayo alizaliwa Yesu? Wanakwenda zahanati au nyumbani...: Yesu alizaliwa huko, kati ya ng'ombe. Walikuwa maskini, walikuwa wahitaji. Msisahau kuhusu watoto wenye uhitaji, watafute! Na muwapatie  upendo wenu, chama chenu kiwasaidie.” Papa alisema anavyopenda jambo hilo, kwamba walileta zawadi kuwapa maskini.

Papa na ACR
Papa na ACR

Kwa njia hiyo aliwahimiza kuwa karibu kila wakati, katika sala na mapendo, kwa nani? Kwa wale wanaoteseka, kwa watoto wengi kama wao ambao ni wagonjwa, wenye njaa, vita, na magonjwa. Kuhusiana na vita, watoto wanaotoka Ukraine, ambao waliwaleta ili kuwaondoa kwenye vita hivyo vichafu, Papa aliuliza: “Je mnajua kwamba watoto wa Kiukreni, ambao waliishi wakati wa vita, wamesahau jinsi ya kutabasamu?” Kwa njia hiyo wawafikirie watoto, na  watu hao. Kwa kufanya hivyo wanarudia wimbo wa Malaika: “Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kati ya watu awapendao”(Lk 2:14). Papa Francisko kwa kuhitimisha amewabariki na kuwaomba wasisahau kumwombea.

PAPA NA ACR ITALIA
20 December 2024, 17:06