2024.12.19 Wavietnamu waishio Roma. 2024.12.19 Wavietnamu waishio Roma.  (Vatican Media)

Papa kwa wafadhili wa asili ya Vietnamu:mshikamano na maskini ni kuitikia agizo la Bwana

Tangu nyakati za mitume,washiriki wa Mwili wa Kristo walisaidiana kwa rasilimali zao.Mshikamano wao na maskini na wale wanaoishi pembezoni mwa jamii wanaitikia agizo la Bwana la kujali hata kidogo wa mwisho kati yetu;na kama Mtakatifu Paulo anavyotukumbusha,ni muhimu kwamba usaidizi huu kwa mdogo utolewe kwa moyo wa furaha na tabasamu.Ni Mawazo ya Papa alipokutana na kikundi cha wafadhili wa asili ya Kivietnamu wa Shirika la Kipapa la Wamisionari kutoka Marekani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na kikundi cha wafadhili wa asili ya Kivietnamu wa Shirika la Kipapa la Wamisionari kutoka Marekani, Alhamisi tarehe 19 Desemba 2024. Ni furaha yake kukutana nao wakati wa hija yao jijini Roma ambayo imefanyika siku chache kabla ya kufungua Mlango Mtakatifu, unaoashiria mwanzo wa Mwaka huu wa Jubilei. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba wakati huu utawaruhusu waamini wote kupata uzoefu wa kweli na wa kibinafsi na Bwana Yesu Kristo, ambaye ni lazima kumtangaza daima, kila mahali na kwa kila mtu kama Yesu, tumaini letu (Spes non confundit, 1). Kujitolea kwao kuunga mkono umisionari na kazi za upendo wa Kanisa zima ni kielelezo halisi cha tangazo hilo na kitasaidia kuleta tumaini lililozaliwa na Injili kwa  kaka na dada zetu wengi katika sehemu mbalimbali za dunia.

Papa akutana na wavietnamu waishio Marekani
Papa akutana na wavietnamu waishio Marekani

Tangu nyakati za mitume, washiriki wa Mwili wa Kristo walisaidiana kwa rasilimali zao (rej 2Kor 8:1-15). Mshikamano wao na maskini na wale wanaoishi pembezoni mwa jamii wanaitikia agizo la Bwana la kujali hata kidogo wa mwisho kati yetu; na, kama Mtakatifu Paulo anavyotukumbusha, ni muhimu kwamba usaidizi huu kwa mdogo utolewe kwa moyo wa furaha (rej. 2 Kor 9:7), kwa tabasamu. Bwana awajalie daima kutoa sadaka zao kwa roho ya furaha, na sadaka zao zikazae matunda katika maisha ya kaka na dada zao, ambao kwa hivyo wataweza kuonja upendo mwororo na huruma ya Kristo.

Kundi la Wavietnamu waishio Roma
Kundi la Wavietnamu waishio Roma

Ishara ya Wakatoliki wengi waliohama kutoka Vietnam hadi Marekani ni imani thabiti waliyokwenda  nayo. Papa ana uhakika kwamba inawatia msukumo hamu yao ya kusaidia jumuiya za Kikristo katika nchi zilizo mbali na nychi yao. Kwa hisia hizo, Baba Mtakatifu amewatakia ziara njema ya Roma, ambayo kwa takriban milenia mbili imewakaribisha waamini wanaofika kwenye makaburi ya Mitume na mahali pengine patakatifu. Safari hii iwafanye upya katika imani na iwaimarishe katika kutoa sadaka. Amewabariki kwa moyo wote na familia zao na amewaomba tafadhali wasisahau kumuombea.

Kundi la wavietinamu waishi Marekani
Kundi la wavietinamu waishi Marekani
Wafadhili wa kivietnamu waishio Marekani
19 December 2024, 15:59