2024.12.10 RWANDA: Kongamano la II la  Ekaristi Kitaifa. 2024.12.10 RWANDA: Kongamano la II la Ekaristi Kitaifa. 

Papa atuma ujumbe kwa Washiriki wa Kongamano la II la Ekaristi,Rwanda

Katika Ujumbe wa Papa Francisko,uliotiwa saini na Kardinali,Pietro Parolin,Katibu wa Vatican anahimiza kazi ya washiriki wa Kongamano la Pili la Ekaristi Kitaifa lililofanyika nchini Rwanda kuanzia tarehe 4 hadi 8 Desemba 2024 kuwa Ishara ya Matimaini yanayoonekana baada ya Mungu wa Utatu na asili yake ya uhusiano.Ndani yake watu katika jumuiya wanakusanyika,wakivunja vizuizi vya rangi,lugha au utamaduni na kuwa wamisionari wa udugu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Ujumbe uliolekezwa kwa Askofu Vincent Harolimana, wa Jimbo la  Ruhengeri,na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Rwanda (CEPR) kwa ajili ya  Kongamano la II la Ekaristi Takatifu kitaifa lililoanza tarehe 4 hadi 8 Desemba 2024, Baba Mtakatifu Francisko anaungana kwa furaha na shukrani za waamini wote wa Kikristo katika Nchi hiyo ya Afrika. Ujumbe wake uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, Papa anasisitiza juu ya  uwajibikaji kwa  kukabiliana na njia ya kimwili na hadhi ya binadamu.

Akitazama Kaulimbiu ya Kongamano hilo isemayo: “Tumkazie macho Yesu katika Sakramenti ya Ekaristi: chemchemi ya matumaini, udugu na amani” Papa Francisko amebainisha kuwa  inatoa fursa ya kutafakari Ushirika, ambao ni kitovu cha maisha yote ya Kikristo na ishara inayoshikika ya upendo wa Kristo kwa wanadamu wote." Kwa njia hiyo kwa kuiishi, kulingana na Papa Francisko, inatuhimiza kujitoa kama zawadi kwa wengine, huku tukifanya kazi kwa makubaliano ya pamoja kujenga ustaarabu wa upendo.”

Kwa kuzingatia Jubilei ya miaka 125 tangu uinjilishaji ulipoanza nchini Rwanda, Baba Mtakatifu Francisko  anawaalika waamini wote nchini humo kuanza tena kwa “Kristo, mkate wa uzima”, huku akisisitiza kuonesha mshikamano kwa yeyote anayejikuta katika mazingira magumu.” "Ni lazima tuwe ishara dhahiri za tumaini," kwa kuchukua maneno kutoka katika Hati iliyotangaza Mwaka mtakatifu, 2025 ya Spes non confundit,” yaani Matumaini hatakatishi tamaa. Baba Mtakatifu aidha alibainisha " Ekaristi inakumbusha wajibu wa kawaida kuelekea mahitaji ya kimwili na ya kiroho ya binadamu, huku ikichochea matumaini katika Utatu." Asili yake "kimsingi ya uhusiano inaalika watu kuishi katika jumuiya,  badala ya kutengana. Na kwa hiyo kuishi Umoja, kuvunja vizuizi vya kikabila, lugha utamaduni, alihitimisha.

PAPA RWANDA/JUBILEI 2024
10 December 2024, 17:19