Ziara ya Papa huko Ajaccio:Tuombee amani nchi Takatifu na waathirika

Kabla ya kusali sala ya Malaika Bwana huko Ajaccio,mwisho wa mkutano katika Kanisa Kuu la Mama Yetu Mpalizwa na Maaskofu,Mapadre na Watu waliowekwa wakfu, Papa alikumbuka migogoro ambayo imemwaga damu na kuwaombea waathiriwa wa kimbunga kilichokumba visiwa vya Ufaransa vya Mayotte huko,Bahari ya Hindi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Halikuwa dirisha la kawaida linalotazama Uwanja wa Mtakatifu Petro na hapakuwapo na maelfu ya watu wanaosikiliza katika sauti za wasemaji. Lakini ni katika Kanisa lililokiwa tulivu, ambapo maneno ya Papa Francisko yalisikika kwa ukali sana. Popote risasi na mauaji yanapofanyika kutoka Mashariki ya Kati hadi Ulaya, hadi Asia na haya yote ni maeneo ambayo Papa alikumbuka katika orodha hiyo ya maombi ambayo yalifanywa kila Dominika na hayakukosa.

Papa Francisko na Kanisa mahalia
Papa Francisko na Kanisa mahalia

Kwa hiyo maneno hayo pia yamesikika kutoka Ajaccio mwishoni mwa asubuhi ya Ziara yake ya 47 ya Kitume, Dominika tarehe 15 Desemba 2024. Baada ya kuhutubia mapadre na watu waliowekwa wakfu mahalia, Baba Mtakatifu Fransisko alirudia ombi lake la amani mbele kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana Papa alisema:

 

“Sasa tugeukie Bikira Maria kwa maombi. Katika Kanisa Kuu hili lililopewa jina la Mama Yetu wa Kupalizwa, wamini wanaomba upendeleo wake chini ya jina la Mama wa Huduma, "Madunnuccia." Kutoka katika kisiwa hiki cha Mediterania, tumwinulie ombi letu la amani: amani kwa nchi zote zinazozunguka bahari hii, hasa Nchi Takatifu ambako Maria alimzaa Yesu. Amani kwa Palestina, kwa Israeli, kwa Lebanon, kwa Siria, na kwa Mashariki ya Kati yote! Na Mama Mtakatifu wa Mungu atupatie amani inayotamaniwa sana na watu wa Kiukreni na Kirusi. Vita daima ni kushindwa. Amani kwa dunia nzima!

Papa na Kanisa mahalia
Papa na Kanisa mahalia

Dhana ya vita ambayo siku zote ni kushindwa inaenea hadi kwenye uhasama unaoweza kutokea katika jumuiya za kitawa na parokia. Hatimaye, wazo la mwisho kwa watu walioathiriwa na janga la Kimbunga Chido kilichopiga visiwa vya Mayotte vya Ufaransa katika Bahari ya Hindi na kusababisha vifo vya watu wapatao kumi na tano na zaidi ya majeruhi 25. Kwa wote, Papa Francisko alisema “niko karibu kiroho".

15 December 2024, 15:23