Kwaya ya Sistine huko Mt. Apollinari kwa "Matamasha ya Jubilei"
Vatican News
“Matamasha ya Jubilei- Maelewano ya Matumaini'' yatafanyika katika Basilika ya Kirumi ya Mtakatifu Apollinari Roma katika tukio la nne la muziki kwenye muktadha wa "Jubilei ni Utamaduni. " Dominika tarehe 22 Desemba 2024 saa 11.30 jioni, masaa ya Ulaya kwaya ya Kipapa ya Kikanisa cha "Sistina", inayoongozwa na Mwalimu wa Muziki Monsinyo Marcos Pavan, itafanya programu ya kuwaenzi watunzi wakuu wa mapokeo matakatifu, akiwemo Giovanni Pierluigi wa Palestrina, ambaye kuzaliwa kwake ni alama ya karne ya tano katika mwaka 2025, Monsinyo Lorenzo Perosi na Kardinali Domenico Bartolucci.
Tukio wazi kwa umma
Siku chache kabla ya ufunguzi wa Mwaka Mtakatifu, waaandaji wanasema, "utendaji wa nyimbo za polyphonic utawapa washiriki uzoefu wa kutafakari, kuwaongoza katika kutafakari juu ya fumbo la imani na umuhimu wa muziki kama chombo cha kuinua kiroho na kujitafakari.” Programu hiyo inajumuisha Kuzaliwa kwa upya kwa nyimbo za kisasa za kwaya, kwa kuzingatia mapokeo ya muziki mtakatifu wa Kipapa. Tukio litakuwa la bure na wazi kwa umma, bila kuhitaji kuomba.