2024.12.12 Papa alikutana na Bwana Mahmoud Abbas, Rais wa Serikali ya Palestina 2024.12.12 Papa alikutana na Bwana Mahmoud Abbas, Rais wa Serikali ya Palestina  (Vatican Media)

Papa akutana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas

Rais wa Palestina Bwana Mahmoud Abbas alitembelea mjini Vatican na kukutana na Baba Mtakatifu tarehe 12 Desemba 2024.Katika mazungumzo na Sekretarieti ya Vatican walijadili haja ya kusitishwa kwa mapigano huko Gaza.Akizungumza na Vatican Media,alisema kwamba alimwomba Papa kuendelea kukuza utambuzi wa Nchi ya Palestina katika Jumuiya ya Kimataifa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu  Francisko alifanya mkutano wa dakika 30 asubuhi ya tarehe 12 Desemba 2024 na Mahmoud Abbas, Rais wa Serikali ya Palestina. Akizungumza na Roberto Cetera wa Radio Vatican Media, mara baada ya hapo, Rais Abbas alielezea mkutano huo kuwa ulikuwa wenye matunda, na kuongeza kuwa "kila wakati ninapokutana na Papa, ni kama kukutana na rafiki wa zamani". Hata hivyo ulikuwa ni kwa mara ya kwanza viongozi hao  wawili kukutana ana kwa ana katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Abbas na Kardinali Parolin
Abbas na Kardinali Parolin

 

Kwa njia hiyo Rais Abbas alisema kwamba:"Nilimshukuru Baba Mtakatifu kwa maneno yake ya mara kwa mara kuhusu amani katika Mashariki ya Kati na kwa mshikamano anaouonesha daima na raia wa Palestina ambao ni wahanga wa vita huko Gaza." Aidha aliongeza: kusema kuwa: "Nilimwomba aendelee kukuza kutambuliwa kwa Taifa la Palestina katika jumuiya ya kimataifa. Ikiwa amani itapatikana, hakuna mbadala wa suluhisho la serikali mbili."

Papa na Rais Abbas wa Oalestina
Papa na Rais Abbas wa Oalestina

Taarifa nyingine kuhusu Mkutano mjini Vatican ni “hali mbaya sana ya kibinadamu huko Gaza" ambayo ilijadiliwa katika mikutano hiyo, kama vile matumaini ya kusitishwa kwa mapigano na kuachiliwa kwa mateka wote haraka iwezekanavyo. Jambo jingine muhimu  ilikuwa kuhusu "mchango muhimu wa Kanisa Katoliki kwa jamii ya Wapalestina, ikiwa ni pamoja na juhudi zake za sasa za kibinadamu huko Gaza.

Rais Abbas wa Palestina na Sekretarieti ya Vatican
Rais Abbas wa Palestina na Sekretarieti ya Vatican

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vyombo vya Habari Vatican pia ilibainisha kuwa mijadala hiyo imefunika umuhimu wa kutekeleza suluhisho la  serikali mbili, si kwa vurugu bali kupitia diplomasia na mazungumzo, na umuhimu wa hadhi maalum kwa ajili ya Yerusalemu, ili kwamba iweze kuwa mahali pa urafiki kwa dini kuu tatu za tauhidi. Hatimaye, kuhusu Mwaka Mtakatifu ujao wa Kanisa Katoliki wa 2025 ulijadiliwa, na matumaini yalionyshwa kwamba Mwaka wa Jubilei unaweza kusababisha kurudi kwa mahujaji kwenye Nchi Takatifu.

Kubadilishana kwa zawadi

Mwishoni mwa mkutano wa Papa na Rais Abbas, viongozi hao walipeana zawadi ambapo Papa Francisko alimpatia  Rais wa Palestina zawadi kadhaa, ikiwa ni pamoja na ujumbe wake kwa Siku ya Amani Duniani na Kazi ya kisanii iliyoandikwa  maneno "Amani ni ua dhaifu."

Wakati wa kubadilishana zawadi
Wakati wa kubadilishana zawadi

Rais Abbas naye alimaptia Papa zawadi kadhaa, ikiwa ni pamoja na mchoro ukimuonesha akiwa na Papa na moja inayoonesha Papa wakati wa ziara yake huko Bethlehem mnamo 2014. Pia alimkabidhi Papa sanamu ya Mtakatifu Porphyrius, ambaye ni mtakatifu msimamizi wa  Gaza - zawadi kutoka kwa Patriaki Theophilus, Patriaki wa Kiorthodox wa Ugiriki huko Yerusalemu.

Kubadilishana zawadi
Kubadilishana zawadi
12 December 2024, 16:02